'Technically' nina wasiwasi na Simba SC kupata Matokeo CAFCC Final huko New Amaan Stadium Zanzibar

Hammy36

Guest
Jan 17, 2023
80
84
25
Dar Es Salaam
Kwanini?

1. Tayari Saikolojia ya Wachezaji wa Simba SC iko chini kwani wengi Wao baada ya Mechi ya Kwanza Morocco kumalizika na hata majuzi walivyokuwa wakirejea Uwanja wa Ndege JNIA walikuwa wakisema Berkane FC watakiona cha Moto kwa Mkapa kwani Wao wakijua tu wanacheza kwa Mkapa huwa wanakuwa na Morali ambayo haielezeki.

2. Kocha Fadlu Davis na Benchi la Ufundi la Simba SC walikuwa tayari na Maandalizi ya Uwanja wa Mkapa ambao wanaujua vyema kuliko wa Amaan Zanzibar ambao huutumia kwa mara chache.

3. Viongozi wa Simba SC pamoja na wa Serikalini Kiufundi wamechangia mno kuharibu Saikolojia ya Wachezaji wa Simba SC kwa kuonyesha kuwa hata Wao hawautaki / hawakuutaka Uwanja wa Amaan Zanzibar kwa kuwa busy kufanya Ushawishi wa nguvu Kubwa CAF pamoja na Matamko ya kila aina ili tu CAF waruhusu Mechi ipigwe kwa Mkapa Dar es Salaam Tanzania.

4. Suala / Sakata la Uwanja limechelewesha Timu kufanya Maandalizi ya Kimkakati (ya Ndani na Njema) kuuendea huo Mchezo na kwa ambao kidogo tulishawahi Kutumika katika Maandalizi ya Kimafia ya Mechi za Kimataifa (hasa za Simba SC msimu wa 2012/2013) tuna wasiwasi mno.

5. Kipaumbele cha Uongozi wa Simba SC ulikuwa ni kupata Mapato ya Kukufuru kama Mechi ingechezwa kwa Mkapa Dar es Salaam (Tanzania Bara) na hakikuwa kuiandaa Timu vyema.

6. Sina uhakika kama Wachezaji wote wa Simba SC waliweza kuusoma Uwezo na Udhaifu wa Berkane FC zaidi ya Wao wote Kushangilia baada ya kufungwa Goli 2 kwa 0 (ambazo GENTAMYCINE naziita ni za Kizembe mno) kwa Wachezaji kukosa Umakini na kutaka kuonyesha kuwa wako juu ya Berkane FC kiuwezo wakati Kiuhalisia Watu wote wa Mpira tunajua kuwa Simba SC (pamoja na kufika CAFCC Final) bado ni Underdog mbele ya Berkane FC.

7. Wana Simba SC (kuanzia Msemaji), Uongozi na hata baadhi ya Watu katika Benchi la Ufundi kukataa kupokea USHAURI KUNTU kutoka kwa Wadau. Kwa mfano nilihoji sana hapa kuwa kwanini Kiungo Fabrice Ngoma ambaye ni Slow na anakabia Macho anaanza mbele ya Kiungo Deborah Fernandez ambaye ana Vitu vingi vya ziada nikaishia Kudhihakiwa na Kutukanwa.

Siku zote (Watu wa Mpira na tuliocheza Mpira hata wa Ndondo na wa Mashuleni au Vyuoni) tunajua kuwa ukiona tu Kiungo wa Ukabaji kama Yusuf Kagoma anahangaika sana huku muda mwingine akiamua Kufika (kucheza Rafu) jua ya kwenda Kiungo wa Ushambuliaji Fabrice Ngoma hatimizi Majukumu yake, ila wana Simba SC wengi kwakuwa tayari Masikioni na Machoni mwao wana Mahaba na Fabrice Ngoma kamwe hawawezi kuona Mapungufu yake makubwa ambayo kwa nyakati nyingi Huigharimu Timu.

Yangu ni haya tu na Karibuni katika Kunitukana kama kawaida yenu hasa mkiambiwa Ukweli ila nina wasiwasi mno na hii Mechi ya Fainali ya Pili Amaan Stadium Zanzibar kama tutashinda ila kwa Berkane FC ambao nimewaona Kiufundi nina uhakika kuwa bado hata hiyo Mechi watatufunga na hata kama Simba SC tushinda basi ni kwa Goli Moja (1) tu ambalo pia litakuwa ni Furaha kwao kwani watakuwa Mabingwa wa CAFCC 2024/2025.
 

Skr_tz

Mgeni
Jul 2, 2024
12
4
5
Tunaheshimu mawazo yako. Lakini, kabla hujawakosoa Simba na udhaifu wao kumbuka kilichomkuta Yanga na mamelodi. Hadithi ni Ile Ile msimuliaje tu ndio amebadilika.
 

Nzagule1993

Mpiga Chabo
May 20, 2025
1
0
0
Subirini Simba Washinde Ndio Utajua Ni Underdog au Nini Kwasasa Hakuna Mchambuzi anayeipongeza Simba Ila Subirini Ukuu Wa Mungu Ujitokeze Huko Huko Zanzibar
 

Skr_tz

Mgeni
Jul 2, 2024
12
4
5
Subirini Simba Washinde Ndio Utajua Ni Underdog au Nini Kwasasa Hakuna Mchambuzi anayeipongeza Simba Ila Subirini Ukuu Wa Mungu Ujitokeze Huko Huko Zanzibar
Hakika kwa kweli. Wao wamefanya figisu za wazi. Na Simba huwezi kujua watajipanga kwa namna gani. Kikubwa tusubiri siku ifike maneno yasiwe mengi.
 

Ahmed mkamba

Mpiga Chabo
May 20, 2025
1
0
0
Post ako 80% imejaa ushabiki na hujazungumzia soccer na imenipa mashaka hata huo mpira ulocheza shuleni labd ni mpira wa vikapu., nakukumbusha tuu timu ikishafika fainali basi jua hakuna underdog kwa mechi hyo ndo mana hata man city kafa kwa crystal palace fainali juzi ukitaka kuwa mwandishi mzuri mapenz weka pembeni