Hatimaye sakata la wachezaji watatu nyota wa timu ya Singida Black Stars (SBS) kupewa uraia wa Tanzania, limetinga kortini.
Wakili Peter Madeleka amefungua kesi ya kikatiba akidai utoaji huo wa uraia ulikiuka Katiba ya Tanzania.
Kesi hiyo ya kikatiba imesajiliwa Mahakama Kuu Masjala ya Dodoma...