Achana na ukaribu wa Morocco na Hispania ambao ni kilometa 16 tu

Mgunda Zone

Mgeni
Nov 4, 2022
83
88
5
Achana na Timu za Morocco kubeba mataji yote ya CAF Tournaments msimu uliopita (Wydad na Rs Berkane)

Achana na Morocco kumpasua Ubelgiji kwenye group stage ya Kombe la Dunia.

Achana na Kocha Walid Regragui alietoka kuchukua Kombe la CAF Champions League akiwa na Wydad Casablanca baada ya kumpasua Pitso Mosimane akiwa na Al Ahly mpaka kuwa Kocha pekee alieivusha timu kutoka Afrika kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia mwaka huu pale Qatar.

Achana na story za mama yake na Achraf Hakimi kufanya kazi za ndani nchini Hispania alikomzaa Achraf.

Njoo hapa....
Kati ya wachezaji 11 wa Timu ya Taifa ya Morocco walioanza kwenye Kikosi cha kwanza ni wachezaji 3 tu ndio WAMEZALIWA nchini Morocco.

Youssef En-Nesry,Azzedine Ounahi na Nayef Aguerd ndio wachezaji pekee waliozaliwa nchini Morocco.

Yassine Bounou - Canada🇨🇦
Achraf Hakimi - Hispania🇪🇦
Romain Saiss - Ufaransa🇲🇫
Noussair Mazraoui - Uholanzi🇳🇱
Sofyan Amrabat - Uholanzi🇳🇱
Selim Amallah - Ubelgiji🇧🇪
Hakim Ziyech - Uholanzi🇳🇱
Soufiane Boufal - Ufaransa.🇲🇫

Morocco wakiwa na kikosi hiki,mara ya mwisho kufungwa ndani ya dakika 90 ilikuwa mwaka October 15,2019 walipokufa 3-2 kutoka kwa Gabon japo kwenye kikosi hicho ni Hakimi na Amrabat tu aliekuwepo.

#NB: Pengine jana ndio siku pekee Waafrika wamewashangilia Waafrika wenzao wa Kaskazini (Waarabu) maana huku kwenye AFCON huwa tunajua kinachotokea!