Al Ahly uso kwa uso na Madrid

Feb 7, 2023
61
36
5
Miamba ya soka barani Afrika Al Ahly ya Misri wataingia uwanjani hii leo kuvaana na mabingwa mara nyingi wa ulaya Real Madrid katika michuano ya klabu bingwa duniani.
Al Ahly wameingia kwenye michuano hii akiwa mshindi wa pili wa klabu bingwa Afrika baada ya kupoteza kwenye fainali dhidi ya Wydad Casablanca, ambaye yeye aliingia kama muandaji wa michuano hii inayofanyika nchini Morocco, wakati Real Madrid ameshiriki akiwa bingwa wa ulaya.
Bingwa huyo mara 10 kwenye michuano ya Afrika amefanikiwa kuingia hatua hii ya nusu fainali mara tatu mfululizo huku akiishia kwenye hatua hiyo mara zote,wakati Real Madrid yeye amefanikiwa kutwaa taji hilo kila akifanikiwa kushiriki michuano hiyo.
Kumbuka Tp Mazembe pekee ndio timu kutoka Afrika iliyofanikiwa kucheza fainali ya klabu bingwa duniani, mwaka 2009 dhidi ya Inter Milan na kupoteza kwa magoli 3-0.
Ipi nafasi ya mwakilishi kutoka Afrika Al Ahly, je anaenda kuvunja mwiko wa kutokuingia fainali au ataendeleza rekodi ya kuishia hatua hiyo dhidi ya Madrid?.
 

Attachments

  • 20230208_130328.jpg
    20230208_130328.jpg
    179 KB · Somwa: 0
  • Like
Reactions: McRay