Ambacho hakizungumziwi na vijana wangu ninaowasoma mitandaoni ni suala la fitness ya Mayele na Yanga kwa ujumla.

Brenda

Mgeni
Oct 31, 2022
489
403
5
Dar es salaam
💫.... Ambacho hakizungumziwi na vijana wangu ninaowasoma mitandaoni ni suala la fitness ya Mayele na Yanga kwa ujumla.

Mayele anasifiwa kufunga tu. Hasifiwi fitness yake. Sijui kwanini. Bao la kwanza jana baada mpira wa kichwa kugonga mwamba reaction ya kufunga kwa mguu ilitokana na fitness yake.

Wengine kuurudia tena ule mpira ni issue kama fitness level yako ipo chini. Bao lake la pili angalia alivyokimbia kwa kasi hatua 25 huku mpira ukiwa kwa Aziz Ki. Mbele yake kulikuwa na mabeki wawili wa Coastal, akawapita, na bado hawakuweza kumechi na kasi yake.

Wakati mwingine mabao yake yanatokana na fitness aliyonayo. Yule jamaa mwenye minywele benchi la Yanga ni mtu muhimu sana. Wachezaji wengi wa Yanga wako fiti kimwili hata kabla ya suala la akili zao uwanjani.