Arsenal, City kuamua hatma ya Ubingwa leo

Feb 7, 2023
61
36
5
Majira ya saa 4:30 usiku wa leo kutakuwa na mbungi ya kuamua mbio za ubingwa kati ya Arsenal dhidi ya Man city katika dimba la Emirates.

Mechi hiyo inatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na ubora wa timu zote mbili,huku wote wakiwa wanashindania ubingwa.

Arsenal yupo kileleni kwa alama 51,michezo 21 huki City wenyewe wana alama 48 na michezo 22, hivyo ushindi wa City leo utawafanya kupanda mpaka kileleni kwa tofauti ya magoli ya kufunga (City 56, Arsenal 46).

Arsenal nae haitaji kingine zaidi ya alama muhimu kwake ili kuendelea kusalia kileleni huku bado akiwa na mchezo mmoja mkononi.

Utamu mwingine wa mechi hii ni inawakutanisha kati ya Mwalimu (Pep) na Mwanafunzi wake (Arteta) huku Arteta akiwa amepoteza mechi zote tano za mwisho dhidi ya City.

Mbinu za makocha na ubora wa wachezaji zitaenda kuamua mchezo leo
20230215_162826.jpg
 
  • Like
Reactions: Kriss and Lukac