Arsenal vs Manchester United mechi bora ikisindikizwa na magoli 5 🔥⚽️

Nabi

Mgeni
Nov 4, 2022
121
124
5
Arsenal inazidi kuthibitisha ubora wake kwenye EPL msimu huu baada ya jana kushinda mechi yake na Manchester United.

Kama isingekuwa makosa madogo madogo ya Arsenal ya kupoteza mipira kwenye eneo lao la kushambulia, basi nadhani wangeweza kushinda goli zaidi ya 3.

Pongezi kwa Mikel Arteta kwa kubalance kikosi cha kwanza vizuri sana, ametengeza uwiano mzuri sana kwenye kila eneo yani safu ya ulinzi, safu ya kiungo na safu ya ushambuliaji, bila kusahau Ramsdale anafanya kazi nzuri sana golini.

Usajili wa Trossard ni wenye tija sana kwenye timu ya Arsenal, amecheza dakika kama 10 tu, lakini ameonesha kitu kikubwa sana kwenye mchezo wa jana.

Manchester United walikosa muunganiko kutokea kwenye eneo la kati, hii ni kutokana na viungo wao kuzidiwa na viungo wa Arsenal, tatizo hilo la kukosa muunganiko kwa Manchester United lilipelekea safu ya ushambuliaji kukosa mipira mingi ya kuweza kufunga magoli, mfano kwa mshambuliaji mpya wa Manchester United, Weighorst ilifaa apatiwe mipira mingi ya krosi za juu, kwa urefu alionao, bila shaka angeweza kupeleka madhara makubwa kwa safu ya ulinzi ya Arsenal.

Ukiachilia mbali Manchester United kupoteza mchezo wa jana, lakini timu inaonesha kuimarika siku hadi siku, pongezi nyingi sana kwa Ten Hag.

Bila shaka kila mpenzi wa soka alifurahia sana mchezo wa jana, ilikuwa bonge la mechi.