AZAM SC

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Mmarekani wa Azam Atangaza Kuutaka Ubingwa wa Simba.​

AZAM-1.jpg

KOCHA Mkuu wa Azam raia wa Marekani, Abdi Hamid Moallin ameweka wazi kuwa kipaumbele chake kikubwa
mara baada ya kurasimishwa kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho, ni kuhakikisha wanashinda ubingwa wa
Kombe la Shirikisho laAzam (FA) linalotetewa na Simba.
Moallin alitangazwa rasmi kuchukua majukumu ya ukocha mkuu ndani ya kikosi chaAzam
Januari 25, mwaka huu mara baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa mafanikio kama kaimu kocha mkuu tangu Desemba mwaka jana.
Tayari chini yakeAzam kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho laAzam wamefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora mara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa hatua ya 32 bora dhidi ya Transit Camp, ambapo sasa watavaana na Baga Friends.
Akizungumza na Championi Jumatano, Kocha Moallin alisema: “Ni jambo zuri kuona kikosi chetu kimefanikiwa kufika hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho, tunayo malengo mengi kama timu msimu huu.
“Lakini lengo kubwa la muda mfupi ni kuhakikisha tunapata nafasi ya kucheza fainali ya michuano hii na kutwaa ubingwa, ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kucheza mashindano ya kimataifa mwakani.”
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Dube: Nimerudi Kuwafungia Mabao Azam FC.​


BAADA ya kupitia kipindi kigumu cha kuandamwa na majeraha, hatimaye straika wa Azam FC, Prince Dube,
amesema kuwa kwa sasa yupo fiti, anataka kupambana na kuifungia mabao mengi timu yake.
Dube amesema msimu uliopita alipishana na kiatu cha ufungaji bora kwa sababu alikuwa anaumia mara kwa mara, lakini kwa sasa yupo fiti na anarudi akiwa na nguvu kubwa uwanjani.
Akizungumzia hali yake kiafya na mwenendo wa ligi tangu kuanza kwa msimu huu, Dube alisema kumekuwa na mabadiliko makubwa kwa timu nyingi na ushindani umeongezeka, ila kwa kuwa amepona na kuwa fiti, atafanya kile mashabiki wake wanataka.
“Msimu niliuanza vibaya kutokana na majeraha. Niliumia sana kwa sababu malengo yalikuwa ni kuisaidia timu
ila nashukuru nimerejea na nipo tayari kwa hilo,” alisema.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Azam FC Yawapa Somo Yanga.​

azam.jpg

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Azam FC Thabith Chumwi Zakaria ‘Zaka Zakazi’ ameingilia kati sakata la Malalamiko ya Waamuzi lililoibuliwa na Young Africans Jumanne (Februari 08).
Idara ya Habari na Mawasilino ya Young Africans ilifanya Mkutano na Waandishi wa Habari na kuweka hadharani namna wanavyosikitishwa na maamuzi ya baadhi ya waamuzi waliochezesha michezo yao msimu huu 2021/22.
Jana Jumatano (Februari 09), Wazee wa Young Africans nao walitilia mkazo sakata hilo, kwa kuzungumza na Waandishi wa Habari huku wakiomba kuonana na Rais Samia ili kufikisha kilio chao cha waamuzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kutokana na hali hiyo, ‘Zaka Zakazi’ amejiunga kwenye hoja hiyo kwa kuiingiza klabu yake ya Azam FC kwa madai ya kunyimwa haki na waamuzi katika michezo kadhaa, hadi kufikia hatua ya kushindwa kufikia malengo iliyojiwekea.
‘Zaka Zakazi’ ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii (Instagram na Facebook) kuendeleza mjadala huo, huku akiwataka Young Africans kuwa wapole, kwani hata Azam FC imekua ikipitia hali ya kunyimwa haki inapokua kwenye mapambano ya alama tatu za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ ameandika: YANGA MMEELEWA AZAM FC INAKWAMA WAPI?
Nafasi moja tu ya kufunga dhidi ya Mbeya City imewaibua watu wakubwa kama waziri Mwigulu, wasemaji, wahamasishaji na wazee wa Yanga na kutaka kuonana na Rais wa nchi.
Niwakumbushe tu kwamba haya mambo @azamfcofficial inakutana nayo kila msimu.
Azam FC hupoteza alama zaidi ya 15 kila msimu kwa mambo kama haya.
Kunyimwa penati, kukataliwa magoli, kuzimwa mashambulizi na hata wapinzani kupata penati au mabao yasiyo sahihi.
Msimu huu peke yake Azam FC imekataliwa penati tano, moja ikiwa dhidi yenu Yanga.
Haya huwa yanatokea katika kipindi ambacho mbio za ubingwa zimechanganya
Mbaya zaidi wakati Azam FC inakutwa na haya, wapinzani wake kwenye mbio za ubingwa wanapata magoli kona, na mambo mengine yasiyosemekana.
Hebu fikiria wakati Azam FC imekataliwa penati tano msimu huu, halafu Simba wanapata penati kama ile dhidi ya Tanzania Prisons au bao kama lile dhidi ya Mbeya Kwanza.
Au nyingi Yanga mnapata penati kama ile dhidi ya Ruvu Shooting au Namungo.
Sisi tunapambana tuwakamate walioko juu yetu, lakini hawakamitiki kwa sababu ya haya mambo.
Mwisho wa msimu Azam FC inakuwa ya tatu halafu swali linakuwa, MNAFELI WAPI?
Kama sisi tungesema twende kwa Rais na kumpelekea kila kosa tunalofanyiwa kwenye huu mpira wetu, basi angetumia muda mwingi sana kuhangaika na matatizo yetu badala ya matatizo ya watanzania kwa ujumla.
Hapa ndipo Azam FC inakwama. Nadhani sasa mtakuwa mmeelewa.
Ahsanteni sana!
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Moallin awaza ku​

vunja ufalme wa Simba, Yanga, Sakho amstua.​

moalin pic

KITENDO cha kuota nyasi kibarua cha Mzambia George Lwandamina katika timu ya Azam FC ilikuwa ni neema kwa Abdihamid Moallin ‘Master Lecturer’ ambaye mabosi wa timu hiyo walimteua kusaidiana na Mohamed Badru kukiongoza kikosi hicho.
Awali, Moallin alikuwa akihudumu Azam kwa wiki kadhaa kama mkurugenzi wa ufundi wa kituo cha kukuza vipaji, huku Badru akiwa kocha wa vijana hao ambao wamegawanyika katika makundi tofauti.
Mbali na kuwa na jukumu la ukurugenzi wa ufundi alikuwa akitumika kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo kama mchambuzi wa mechi (analyst), aliwajibika kufanya kazi kwa karibu na Lwandamina kabla ya kufungashiwa virago.
Mabosi wa timu hiyo waliona Moallin na Badru wanatosha kubeba jukumu la Mzambia huyo kwa muda wakati wakiangalia nani ya kumbebesha mikoba ili awarejeshe kwenye mstari kufuatia kuwa na mwenendo mbaya Ligi Kuu.
Moallin alionekana kumudu hilo kiasi cha mabosi wa Azam kuona anatosha kuwa kocha wa moja kwa moja wa timu hiyo na mwishowe wakampa mkataba wa miaka mitatu na kubatizwa jina la Master Lecturer kutokana na kile alichokifanya kwenye kikosi kipindi kifupi.
Mwanaspoti lilifanya mahojiano maalumu na kocha huyo ambaye amewahi kufanya kazi kwenye Ligi Kuu ya Soka Marekani (MLS) katika timu ya Columbus Crew (2014-2016) kama kocha msaidizi wa timu hiyo na timu za vijana.
Moallin anafunguka mengi ikiwemo ubora wa viwango vya Simba na Yanga kwenye vita ya ubingwa huku akilinganisha na kikosi chake, kuondoka kwa Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na ujio wa Ibrahim Ajib ‘Cadabra’ kikosini.

KILICHOMVUTA CHAMAZI
Wakati akiwa na timu ya Horseed ya Somalia, Moallin anasema alikuja Tanzania kucheza kuwania nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Afrika dhidi ya Azam, lakini cha ajabu ni mazingira ambayo alikutana nayo.
“Yalikuwa mazingira mazuri ambayo kiukweli yalinivutia sana hasa upande wa miundombinu. Nilisema hii ni klabu inayojitosheleza. Niliendelea na mipango ya mchezo lakini bahati mbaya tulitolewa,” anasema. Baada ya kuondolewa kwa jumla ya mabao 4-1, kocha huyo anasema ulikuwa mwanzo wa uhusiano baina yake na Azam FC na kwa wakati huo hakuwa na mawazo kuwa atapata kibarua cha kufanya kazi ndani ya klabu hiyo.
“Hakuna ambaye anaweza kuijua kesho yake ndicho kilichotokea kwani mawasiliano yaliendelea na mwishowe walipendelea niwe sehemu ya klabu yao kwa kujikita kwenye maendeleo ya soka la vijana,” anasema.

KUONDOKA LWANDAMINA
Moallin anasema hakufurahia kufungashiwa virago kwa Lwandamina, lakini anaamini ulikuwa uamuzi ambao ulizingatia maslahi ya pande mbili kutokana na mwenendo wa timu.
“Wakati mwingine kwenye mpira kuna mambo ambayo hutokea bila kutarajiwa. Kama ukurasa ulishafungwa na maisha mengine yanaendelea,” anasema.

ABADILI UPEPO
Moallin anasema baada ya kukabidhiwa timu ili kukaimu nafasi ya Lwandamina alianza kutekeleza majukumu kwa kukaa na mchezaji mmojammoja ili kurejesha morali ya timu kabla ya kuanza kufanyia kazi falsafa za kucheza soka safi la kushambulia kwa kasi. “Haikuwa rahisi lakini nashukuru Mungu kwa sababu kila kitu kilienda vizuri na wachezaji walikuwa tayari kubadili mwelekeo wa timu. Nilijitahidi kumfanya kila mchezaji ajisikie kuwa sehemu ya timu. Kila ambaye alionyesha nilimpa nafasi na ndio siri iliyoturejesha kwenye mstari,” anasema.

NAFASI YA MAKINDA
Kocha huyo anasema umri sio kigezo cha mchezaji kupata namba ya kucheza kikosini, badala yake kipaumbele chake ni uwezo.
“Mchezaji yeyote anaweza kupata namba kwenye kikosi changu, kikubwa ni kuona vile anaweza kuyabeba majukumu na kutekeleza,” anasema Moallin.
“Siwezi kumnyima nafasi mchezaji eti kwa sababu ya udogo wa umri wake na kama ni hivyo, basi Tepsi (Evans) asingekuwa anapata namba kwenye kikosi changu. Navutiwa na uchezaji wake na yeyote ambaye atafanya zaidi atakuwa chaguo langu.”
Katika kusaidia vijana, Moallin anasema amekuwa akiwajengea uwezo na kuwaonyesha njia ambavyo wanaweza kutimiza ndoto zao.
“Nipo mstari wa mbele kusaidia wachezaji wanaochipukia kwa faida ya Azam kwa miaka ijayo na hata Tanzania kwa ujumla. Hilo lipo mikononi mwangu.”

AJIBU NI BALAA
Muda mfupi baada ya kuachwa na Simba na kutua zake Azam FC, kiwango cha Ibrahim Ajibu kimemkuna kocha huyo anayesema anatarajia makubwa zaidi kutoka kwa fundi huyo ambaye aliwahi kuwika kwa nyakati tofauti Simba na Yanga. “Anaonekana kuwa ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa. Kiukweli nimevutiwa na kiwango chake. Nataka kumfanya awe huru zaidi ili awape furaha mashabiki wa Azam na akawe na faida kwenye timu,” anasema Moallin.

SURE BOY
Akimzungumzia kiungo wa zamani wa Azam Abubakar salum ‘Suare Boy’, kocha huyo anasema: “Sikupata bahati ya kufanya naye kazi maana nakumbuka kipindi kile alikuwa na adhabu. Pia sikuwa kwenye nafasi ya kufanya lolote, lakini nikiri kuwa ni mchezaji mzuri na mwenye heshima kubwa.”



MBIO ZA UBINGWA
Licha ya uwepo wa tofauti ya pointi 12 kati yao Azam FC na vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga, Moallin anasema wanachokifanya ni kama kumkimbiza mwizi kimyakimya.
Kocha huyo anaamini kuwa lolote linaweza kutokea mbeleni, hivyo wanapaswa kuweka mkazo kila mchezo mbele yao ili kuhakikisha wanajikusanyia pointi za kutosha zitakazowasaidia kufikia lengo mwisho wa msimu.
“Bado tuna nafasi ya kupigania ubingwa. Nimezungumza na wachezaji wangu na kuwaeleza kuwa sisi ni washindi na tunapaswa kuthibitisha hilo. Haijalishi kuwa utofauti wa pointi ni mkubwa kwa kiasi gani, shabaha yetu inatakiwa kuwa kwenye kukusanya pointi,” anasema.
“Hizi ni mbio ndefu ambazo lolote linaweza kutokea mbeleni. Tunatakiwa kuona kuwa ligi ni kama inaenda kuanza hivyo nafasi ipo wazi kwa kila timu.”

SIMBA, YANGA ZIJIPANGE
Kuhusu ubora wa Yanga na Simba, Master Lecturer anasema hilo wala halimnyimi usingizi kwani anaamini ana kikosi bora na kipana ambacho kinaweza kukabiliana na timu yoyote kwenye ligi bila tatizo lolote.
“Nataka kuifanya Azam kuwa timu tishio sio kwa ligi ya ndani tu, bali hata kwenye mashindano ya kimataifa. Taratibu watu wataona kiuhalisia hiki ninachosema. Hakuna timu ambayo inaniumiza kichwa ni suala la muda tu,” anasema.
Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Azam wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi 24 walizovuna kwenye michezo 14, wakiachwa pointi saba na Simba ambao
wana mchezo mmoja mbele huku wakiwa na pointi 31 katika nafasi ya pili.

SAKHO AMSTUA
Mchezaji hatari ambaye amemstua Moallin kwenye ligi ni Pape Sakho wa Simba na anasema dawa yake inachemka maana alimsumbua kwenye michezo yote miwili ambayo amekutana na Simba ukiwemo wa fainali ya Mapinduzi.
“Ni mchezaji hatari sana yule. Kasi yake ilitupa wakati mgumu jinsi ya kukabiliana naye. Alitulazimisha kufanya makosa,” anasema

UVUMI KUTUA SIMBA
Licha ya tetesi kuwa alikuwa kwenye rada za Simba kufuatia kuondoka kwa Thierry Hitimana, Moallin anasema alikuja nchini kwa ajili ya Azam.
“Azam ndio klabu iliyonifanya kuja Tanzania na nina furaha hapa. Shabaha yangu ni kuifikisha nchi ya ahadi.”

MALENGO YAKE
Kuhusu malengo anasema: “Nataka kuifanya Azam kuwa klabu ya mataji, hilo ndio lengo langu kubwa na hakuna ambacho kinashindikana kwa sababu mpira ni mchezo wa wazi, hivyo kama wao ni bora basi natakiwa kuwaandaa vijana wangu kuwa bora zaidi yao.
“Hatuna sababu ya kushindwa. Najua mashabiki wetu wanatamani kuona tukitimiza hilo, hivyo niwatoe shaka kuwa hatutakuwa washiriki tu kwa maana ya kusindikiza klabu nyingine kutwaa mataji.”

MAKOCHA WALIOPITA AZAM
Athuman Kikila (2004), Mohamed Seif ‘King’ (2004–2008), Neidar Dos Santos (2008–09), Itamar Amorin (2009–10), Sylvester Marsh walikuwa kocha wa muda (2010), Stewart John Hall (2010–12), Vivek Nagul (muda) (2012).
Boris Bunjak (2012), Hall alirejea tena Chamazi (2012–13), Joseph Omog (2013–2015), George ‘Best’ Nsimbe (muda) (2015), Hall urejeo wake wa awamu ya tatu (2015–2016), Zeben Hernandez (2016), Aristica Cioaba (2017–2018)
Hans van der Pluijm (2018–2019), Meja Mstaafu Abdul Mingange (muda) (2019), Etienne Ndayiragije (2019), Aristica Cioaba akarejea tena (2019–2020) na wa mwisho kabla ya Moallin ni Mzambia, George Lwandamina (2020-2021).
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Azam ndo kwanza asilimia 60.​

azam pic

AZAM FC imezidi kunoga baada ya juzi usiku kuisambaratisha Baga Friends ya Pwani kwa mabao 6-0 na kutinga robo fainali ya michuano ya ASFC, huku kocha wake, Abdihamid Moallin akifichua eti mziki wote huo ndio kwanza asilimia 60 tu.
Kwa siku za hivi karibuni tangu Azam iachane na Mzambia George Lwandamina, timu hiyo imekuwa ya moto chini ya Moallin, ikitoka eneo la kati la msimamo wa Ligi Kuu Bara hadi nafasi ya tatu na juzi iligawa dozi nene kwa Baga katika ASFC.
Hata hivyo, Kocha Moallin alisema pamoja na mfululizo wa matokeo ya ushindi na kucheza soka safi, Azam bado haijafika kwenye kiwango anachoitaka icheze na sasa ipo kati ya wastani wa asilimia 55 hadi 65 ya ubora anaoutaka.
“Nafurahishwa na kile wachezaji wanachokionyesha, kila mmoja anajituma na kufuata maelekezo ipaswavyo, huu ni muendelezo wa malengo yetu kwa msimu huu japo bado hatujafikia asilimia 100 ya ubora ninaoutaka,” alisema Moallin.
“Naangalia zaidi mchezo ujao, hivyo nawapa wachezaji mbinu na mazoezi maalumu kuhusu mchezo unaofuata na kwa kufanya hivyo siku hadi siku naamini ubora utazidi kupanda na kuifanya Azam iwe timu tishio hapa nchini,” aliongeza.
Moallin pia alifunguka kuwa siri kubwa ya matokeo chanya inayoyapata Azam kwa sasa ni kutokana na kuwapa elimu wachezaji wake ya kujitambua na kujiamini zaidi.
“Ujue wachezaji wengi hapa Bongo wana woga, wanaamini Simba na Yanga ndio timu bora. Mimi niliwaeleza hawawezi kufanya vizuri kama hawajiamini kuwa ni bora na kuwataka wajiweke namba moja kwanza kisha wengine wafuate na hilo wamelitimiza na limewaongezea nguvu na kujiamini,” alisema.
Katika michezo sita iliyopita, Azam imeshinda yote dhidi ya Mbeya Kwanza 1-0, Tanzania Prisons 4-0, Transit Camp 1-0, Dodoma Jiji 2-0 na Baga Friends 6-0.
Katika mechi hiyo ya juzi iliyoivusha Azam hadi robo fainali ikiungana na Geita Gold iliyoing’oa Mbuni ya Arusha kwa bao 1-0 lililifungwa na George Mpole, mabao ya Azam yalifungwa na Charles Zulu aliyefunga kwa penalti dakika ya 15, kisha Paul Peter akapiga hat trick dakika 18, 20 na 44, kabla ya Paul Katema na Daniel Amoah kuongeza mengine dakika ya 54 na 89.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

MZEE WA UPUPU: Azam FC wamebadilika, Mbombo na Hamahama ni shida.​

azam pic

TANGU ujio wa kocha mpya wa Azam FC, Abdihamid Moallin, timu hiyo imekuwa tofauti kabisa. Inacheza soka safi, inapata matokeo na inafunga mabao mengi.
Kabla ya Moallin, Azam FC ilikuwa haijawahi kupata zaidi ya bao moja kwenye ligi. Ilikuwa imecheza mechi saba, imefunga mabao saba na kufungwa manane. Lakini baada ya Moallin, mabao yanamiminika tu.
Jumla ya mabao 14 yamefungwa kwenye mechi 6 chini ya raia huyo wa Marekani mwenye asili ya Somalia. Katika mechi hizo, Azam FC imeruhusu mabao 5 tu.
Lakini wakati mwingine namba hazitoi picha halisi. Soka ambalo Azam FC inacheza sasa hivi ni kubwa kiasi kwamba hizi namba hazitoshi kuliezea kwa ukamilifu.
Wachezaji wa Azam FC wamebadilika sana, yaani hadi Aggrey Morris sasa hivi anatulizia mpira mgongoni... amini!
Kenneth Muguna, nyota wa Gor Mahia panga pangua kikosi cha Harambee Stars alionekana usajili wa hovyo zaidi chini ya Lwandamina.
Lakini sasa wachambuzi wote Tanzania wanakubaliana kwamba Muguna ni aina ya mchezaji ambaye hajawahi kuwepo nchini katika majukumu ya nafasi yake. Usimguse Tepsie Evans achana kabisa na Rodgers Kola na sijui useme nini kuhusu Ismail Aziz Kader?
Kwa kifupi kila mchezaji wa Azam FC kwa sasa amebadilika na kuonyesha uwezo wa hali ya juu. Watu pekee ambao hawajabadilika ni Idris Ilunga Mbombo na Abdul Haji Omary maarufu kama Hamahama. Hawa watu sijui wana matatizo gani?
Hawana furaha wakiwa na mpira na hawana furaha wakiwa hawana mpira. Hawaonyeshi kabisa kama ni wachezaji wanaostahili kuchezea timu ya Ligi Kuu achana na timu ya kariba ya Azam FC.
Mbombo yaani hata kutuliza mpira kwake ni tatizo. Azam FC inapocheza na Mbombo ni kama inakuwa pungufu kwa mchezaji mmoja. Akipasiwa mpira, hawezi kuulinda... unapotea, halafu hakabi. Sana sana ataanguka chini na kunyoosha mikono kumlalamikia mwamuzi.
Hana mi-kimbio ya kiushambuliaji. Hana uwezo binafsi wa kumtoka mlinzi, lakini zaidi hana kabisa uwezo wa kucheza kwa kuunganisha safu ya ushambuliaji na kiungo (link up play). Wapinzani wala hawapati shida ya kumkaba. Jinsi anavyojiweka tu uwanjani tayari ameshajikabisha.
Mbaya zaidi nafasi za kufunga ambazo anapoteza unaweza unajiuliza, “Mbombo amekutwa na nini?’
Kwa tunaomjua mkongomani huyu tangu akiwa Zambia tunashangaa sana. Mbombo ni straika mabao. Ni straika hasa. Lakini daaah!
Twende kwa Hamahama. Huyu nadhani siyo aina ya wachezaji ambao wanastahili kuwa Azam FC.
Katika maisha yake ya soka akiwa Azam FC ni mara moja tu alikuwa kwenye ubora wa hali juu. Ilikuwa 2019 kwenye mashindano ya Kagame kule Kigali, Rwanda dhidi ya TP Mazembe.
Kile kiwango alichokionyesha siku ile kama angeelendea nacho sasa hivi tungeshamsahau Kapombe kwenye timu ya taifa.
Kocha wake Etienne Ndayi-ragije alimuwekea matumaini ma-kubwa sana kiasi cha kumuweka nje Nicholas
Wadada kwenye mechi mu-himu ya ugenini ya Ko-mbe la Shiri-kisho dhidi ya Triangle ya Zimbabwe.
Nda-yiragije akitafuta matokeo ya kupindua meza, akamuamini Hamahama ugenini. Unaweza kuona ni namna gani alimuona kama kesho ya Azam FC. Lakini hakufanya kitu mbele ya Ndayiragije, na makocha wengine wote waliokuja baada ya hapo.
Aristica Cioaba alipendekeza aondolewe kwa mkopo na kumtaka Salum Kimenya wa Tanzania Prisons, lakini ikashin dikana. Hamahama akabaki akipewa muda wa kuboresha uwezo wake.
Alipokuja George Lwandamina, akamuamini tangu siku ya kwanza na kumuweka benchi Wadada. Lakini muda mchache baadaye akabaini kwamba yaliyomo aliyodhani kayaona kwake kumbe hayamo. Maisha yanaendelea hivyo hivyo kwa Master Lecturer.
Wa-chezaji wote wa Azam FC wako dunia nyingine kasoro hawa jamaa wawili.
Nadhani hata Azam FC wenyewe wanaona na tusitegemee kuwaona wachezaji hawa kwenye jezi za Azam msimu ujao. Hawabadiliki, hawaoneshi hamu ya kubadilika.
Yawezekana wasiwe wachezaji wabaya, lakini Azam FC siyo sehemu yao sahihi.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

AZAM FC YAICHAPA PAMBA FC 2-0 MECHI YA KIRAFIKI​


MABAO ya washambuliaji, Mzambia Rodgers Kola na Mzimbabwe, Prince Dube yameipa Azam FC ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Pamba FC katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
Azam FC imewasili Mwanza jana kuweka kambi fupi kujiandaa na mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Biashara United Februari 22 Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Kumbe Azam Fc Bado Sana​

273256013_1309603512877435_1626923907249693629_n.jpg

AZAM inakamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara lakini kocha wake, Abdi Hamid Moalin, amesema bado hajaipata Azam anayoitaka na ubora wa kikosi chake kwa sasa hauzidi asilimia 65.
Moalin amefunguka kuwa kuna levo ya ubora ambayo anahitaji kuiona kwenye timu yake, jambo ambalo bado analifanyia kazi kwa sasa na atafanikiwa muda siyo mwingi.
“Timu inapata matokeo ya ushindi mfululizo, ila kwetu bado hatujafikia kwenye kiwango ambacho tunahitaji timu icheze na idumu kwenye ubora huo. Nafikiri (kwa sasa) ni kama asilimia ni 55 au 65 tu,” alisema.
Azam imeshinda mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu Bara, haijapoteza mechi yoyote tangu ifungwe na Simba 2-1 siku ya Mwaka mpya.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Dube amekuja kuwashika!​

Dube pic

BAADA ya kusota kwa siku 273 bila kutikisa nyavu hatimaye mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube ametoa gundu kabla ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United unaopigwa kesho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Dube alimaliza na mabao 14 msimu uliopita, akiwa kinara wa timu yake licha ya kutumia muda mrefu nje ya uwanja kujiuguza majeraha na mara ya mwisho kufunga ilikuwa Mei 20 mwaka jana dhidi ya Biashara United.
Ijumaa iliyopita Mzimbabwe huyo aliyeshiriki Fainali za Afcon 2021 zilizofanyika Cameroon, alifunga bao wakati Azam ikiinyoosha Pamba kwa mabao 2-0
kwenye mechi ya kirafiki iliyopigwa Nyamagana, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya kesho dhidi ya Biashara, timu aliyoitungua mara ya mwis ho katika Ligi Kuu.
Azam na Biashara zitaumana CCM Kirumba baada ya Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, uliopo Musoma mkoani Mara kufungiwa kutokana na kukosa vigezo.
Akizungumza na Mwanaspoti, Dube alisema amekaa nje ya uwanja muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ila anafahamu kilichomleta ndani ya timu hiyo kuwa ni kufunga hivyo ni muda wake sasa.
“Nafurahi kuwa miongoni mwa wachezaji wanaoleta furaha ndani ya timu nimefunga hiyo ndio kazi yangu nikipewa nafasi zaidi nitafunga na nitakuwa miongoni mwa wachezaji watakaofunga mabao mengi msimu huu kwa sababu ndio kazi iliyonitoa Zimbabwe na kunileta Tanzania,” alisema Dube na kuongeza;
“Hakuna kitu kinaumiza kuwa nje kwa majeraha.”
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAZOEZI YA MWISHO AZAM KABLA YA KUIVAA POLISI​


WACHEZAJI wa Azam FC wakifanya mazoezi kuelekea mchezo wao wa kesho wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Polisi Tanzania Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

MTU WA MPIRA: Viongozi Azam FC wajitathmini, timu imekwama​

azam pic

IPI timu tajiri zaidi nchini kuliko Azam FC? Hakuna. Si Simba wala Yanga, Azam ndio timu tajiri zaidi hapa Tanzania.
Kwanza inamilikiwa na familia ya bilionea Salim Said Bakhresa. Ni mtu mwenye fedha nyingi. Halafu mbali na hilo, familia hiyo inapenda sana soka.
Hii ndio sababu Azam hadi sasa ndio pekee inayomiliki uwanja wa kisasa. Ndio klabu yenye hosteli. Ndio timu inayomiliki mabasi ghali zaidi ya kubeba wachezaji. Yaani kwa kifupi ina kila kitu.
Fedha ambazo Mohamed ‘Mo’ Dewji amewekeza pale Simba ni za matumizi ya Azam kwa miaka minne au mitano tu. Sh20 bilioni ni fedha ndogo sana kwa Bakhresa. Ndio sababu nakwambia Azam ni timu tajiri.
Wakati Mo Dewji anatoa pesa kama hisani ama msaada katika matumizi mengine pale Simba, Bakhresa anatumia fedha kwa ajili tu ya furaha yake pale Chamazi. Hatoi msaada wala hisani ameamua kuwekeza katika soka. Ni kwa furaha ya Watanzania.
Pamoja na utajiri huu, bado Azam imekuwa timu ya kawaida sana katika ligi yetu. Ilianza kwa kasi katika miaka mitano hadi sita ya mwanzo, lakini sasa mambo yamekuwa tofauti.
Baada ya miaka michache Azam ilikuwa ikizitenganisha Simba na Yanga pale juu kwenye msimamo.
Baada ya miaka michache tu ikawa imetwaa taji la Ligi Kuu Bara. Ikatwaa mataji ya Mapinduzi na Kagame. Ilikuwa tishio kweli. Ni nyakati hizi mtendaji mkuu wa timu alikuwa Nassoro Idrissa ‘Father’. Kwenye benchi la ufundi walikuwepo watu wa soka. Alikuwa Jemedari Said kama meneja wa timu, wakawepo kina Philip Alando na wengineo. Watu wanaoufahamu vyema mpira wa Tanzania.
Chini ya utendaji wa Father, Azam iliishi katika uhalisia wa soka la Tanzania. Ilishindana na Simba na Yanga katika usajili. Ilichukua wachezaji Simba na Yanga. Iliweza kucheza mechi ngumu. Haikuonewa na waamuzi. Ilikuwa ikiishi sayari yake.
Hata hivyo, tangu Father ameachia kiti hicho watendaji wengine waliofuata wamefeli. Pengine zipo sababu za wao kufeli, lakini wengi wanaishi katika uongo uongo ambao unawapoteza na kuwakwamisha.
Mfano mzuri alikuja mtendaji mkuu anayeitwa Abdul Mohammed. Huyu akaamua kuachana na wachezaji wengi wakubwa klabuni hapo kwa madai kuwa wanalipwa fedha nyingi. Akaja na mpango wa kubana matumizi. Akawaondoa wachezaji wengine kwa madai kuwa wamechoka.
Akapunguza posho na gharama za fedha za usajili. Katika zama zake Azam ikaanguka kabisa. Ikapoteza ushindani iliokuwa nao katika ligi. Unakwendaje kubana matumizi kwenye timu ya tajiri? Ni kichekesho.
Uliwahi kusikia wapi watendaji wa Chelsea, PSG na Real Madrid wamekuja na mpango wa kubana matumizi? Moja ya sifa ya timu za matajiri ni kutumia fedha. Unakwenda sokoni unanunua wachezaji wakubwa na unawalipa vizuri. Lakini pale Chamazi mtendaji akaamua kubana matumizi. Baada ya anguko hilo, akaja mtendaji mkuu wa sasa, Abdulkarim Amin ‘Popat’. Nini kimebadilika? Hakuna!
Baada ya miaka minne ya Popat, Azam imeendelea kuwa ileile. Imeshinda taji moja la Kagame na FA. Mataji hayo walishinda katika misimu ambayo wakubwa hawakuwa na habari nayo.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SOMALIA WAMKABIDHI JEZI PRINCE DUBE​

AVvXsEjOxXiStwUuNwPvcyBsaiOHEPH9OEIP77KvdqZMRPc1hkWd7RTt7djxaPkVLQwQT2YXmruaH2edk2ndBJJnao3H14exFIRffILgC-qOJLK1FCuU3d85U9-UBzTG-sRVhISftgCFEgU1bm_OjsLpKeaZwHSCGHkgh26zDRZhDRhMBfzDINxwOf7CsjkO=w512-h640

OFISA wa Shirikisho la SOKA Somalia (SFF), Abdinur Warka akimkabidhi jezi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, mshambuliaji Mzimbabwe wa Azam FC, Prince Dube Mpumelelo leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Warka amekuwa na timu ya taifa ya ya Somalia chini ya umri wa miaka 23, ambayo Machi 23 itamenyana na Eswatini Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kufuzu Fainali za Afrika (AFCON U23).
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Azam Yatua Lindi Kibabe​

azam.jpg

KIKOSI cha Azam FC, kimeshuka mkoani Lindi, kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Namungo utakaochezwa keshokutwa Jumatano. Timu hizo mbili zitakutana kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi, huku Namungo walio kwenye kiwango bora msimu huu, wakiwa nyumbani kuwakaribisha Azam.

Timu hizo kwa sasa zote zina pointi 25, lakini Namungo ipo nafasi ya tatu ikiwa juu ya Azam iliyo nafasi ya nne, kutokana na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa. Mzunguko wa kwanza, Azam iliwafunga Namungo bao 1-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam, bao hilo pekee likifungwa na Mcongo, Idris Mbombo dakika ya 90.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Azam, Thabit Zakaria “Zaka Zakazi”, alisema wanataka kurudi Dar na pointi tatu muhimu.

“Tumeanza safari leo (jana) kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Namungo na tunaenda kupambana ugenini ili kuweza kurudi na alama tatu muhimu nyumbani.

“Wachezaji wote wapo vizuri kuelekea mchezo huo na morali ipo juu ili kuweza kurudi kwenye nafasi yetu Ligi Kuu Bara,” alisema Zaka.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Kocha Azam Aapa Kutibua Ubingwa Yanga​

kocha-azam.jpg

BAADA ya Jumatano kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Namungo, Kocha Mkuu wa Azam, Abdul Hamid Moallin, ameweka wazi kuwa amefurahishwa na ari na upambanaji wa mastaa wa kikosi hicho na kuapa kuwa anataka kuona wanaendeleza hilo katika kila mchezo, hususani mchezo wao ujao dhidi ya Yanga.
Azam ambayo ilicheza michezo mitatu mfululizo bila matokeo ya ushindi, juzi Jumatano walitoka nyuma kwa bao 1-0 na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Namungo, ushindi ambao umewafanya wapande hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo na pointi 28 walizokusanya kwenye michezo 18.
Baada ya ushindi huo, Azam sasa wanajipanga kuvaana na Yanga ambao wanaonekana kudhamiria kushinda ubingwa msimu huu katika mchezo wao ujao wa ligi kuu, uliopangwa kuchezwa Aprili 6, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Kocha Moallin alisema: “Kwanza kabisa nawapongeza sana wachezaji wangu kwa namna ambavyo walipambana katika mchezo wetu uliopita dhidi ya Namungo, ni wazi ulikuwa mchezo mgumu sana kwetu, nadhani tulikuwa tunakosa upambanaji wa namna hii kwenye michezo yetu iliyopita.
“Ninaitaka Azam ninayoifundisha mimi icheze kwa kiwango hiki kwa kila mchezo ulio mbele yetu hususan mchezo dhidi ya Yanga ambao najua ni mchezo mkubwa, lazima tuhakikishe tunatumia faida ya kucheza nyumbani kupata matokeo dhidi yao.”
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
D94E22AD-53B7-4CA0-A706-45E350C1AB71.jpeg

TIMU ya Azam FC itakuwa na mechi ya kirafiki dhidi ya DTB Jumanne Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Kwa Azam, mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wao ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Yanga SC Aprili 6, mwaka huu hapo hapo Azam Complex.
Na kwa DTB mechi hiyo ni ya kujipanga kwa michezo yake ijayo ya ligi ya kuwania kupanda Ligi Kuu, ijulikanayo kama Championship.
Ikumbukwe Yanga wao watakuwa na mechi ya kujipima pia Jumatano hapo hapo Chamazi dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar.
31F19BB9-EBCC-4AE2-A4AE-19D5DA4EE922.jpeg
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

AZAM FC YAICHAPA DTB 1-0 KIRAFIKI CHAMAZI​

62DB3C5D-FBFA-4A47-B072-DE05F1C91288.jpeg

BAO pekee la beki Edward Charles Manyama dakika ya 79, limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya DTB katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

MAZOEZI YA MWISHO AZAM FC KUIVAA YANGA KESHO​




WACHEZAJI wa Azam FC wakiwa mazoezini kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Yanga SC kesho Saa 1:00 usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.





 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Chilunda Kukaa Nje kwa Muda wa Wiki Nne, Daktari Adai Haitaji Upasuaji​


chilunda.jpg

Shaban Chilunda akiwa nchini Afrika Kusini kupata matibabu ya goti
MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Azam FC Shaaban Iddi Chilunda anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki nne baada ya kupata majeraha ya goti katika mchezo wa kirafiki kati ya Azam FC na Dtb.

Chilunda akiongoza na Daktari wa Timu Dkt Mwanandi Mwankemwa wameelekea Cape Town Afrika ya Kusini kwa ajili ya kufanya vipimo vya MRI kutokana na majeraha hayo.

Baada ya kufanyiwa vipimo hivyo amegundulika kupata madhara ya kuumia Mtulinga (Ligament) wa Kati-Pembeni, hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka Klabuni.

chilunda.webp

Chilunda akiwa katika majukumu na Klabu yake ya Azam
Daktari Robert Nicolas kutoka Hospitali ya Orthopaedic Surgeon Vicente Palloti ambaye anamfanyia uchunguzi amethibitisha kuwa Chilunda hana haja ya kufanyiwa upasuaji lakini anatakiwa kae nje ya Uwanja kwa takribani wiki nne baada ya hapo ataanza kufanya mazoezi mapesi na atakuwa amepona kabisa.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
MATCHDAY
Azam Fc
🆚
Simba Sc
🏆
Nbc Premier League
🇹🇿

🗓
May 18, 2022
🏟
Azam Complex
⌚
19:00 PM (EAT)
Nani ataondoka na alama tatu hii leo?
280750218_5356359577757282_718954475692042575_n.jpg
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

AZAM FC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-1 MANUNGU​


TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na Ayoub Lyanga yote dakika ya 20 na 54, wakati bao pekee la Mtibwa Sugar limefungwa na Said Ndemla dakika ya 80.
Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 36 na kupanda nafasi ya nne, ikizidiwa pointi moja na Namungo FC baada ya wote kucheza mechi 25, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 28 za mechi 25 pia nafasi ya 10.