Tafuta
Tafuta vichwa vya habari tu
Kutoka kwa:
Tafuta vichwa vya habari tu
Kutoka kwa:
Nyumbani
Majukwaa
Story Mpya
Tafuta Majukwaa
Story Mpya
Posti Mpya
Posti Mpya za wasifu
Vilivyofanyika
Wanachama
Wanaotembelea kwa sasa
Posti mpya za wasifu
Tafuta Posti za wasifu
Ingia
Jiunge
Tafuta
Tafuta vichwa vya habari tu
Kutoka kwa:
Tafuta vichwa vya habari tu
Kutoka kwa:
Menu
Install the app
Install
Reply to thread
Majukwaa
Maskani ya Michezo na Mikeka
Kijiwe cha Ligi Kuu Bongo
AZAM SC
JavaScript is disabled. For a better experience, please enable JavaScript in your browser before proceeding.
You are using an out of date browser. It may not display this or other websites correctly.
You should upgrade or use an
alternative browser

Message

MZEE WA UPUPU: Azam FC wamebadilika, Mbombo na Hamahama ni shida.

TANGU ujio wa kocha mpya wa Azam FC, Abdihamid Moallin, timu hiyo imekuwa tofauti kabisa. Inacheza soka safi, inapata matokeo na inafunga mabao mengi.

Kabla ya Moallin, Azam FC ilikuwa haijawahi kupata zaidi ya bao moja kwenye ligi. Ilikuwa imecheza mechi saba, imefunga mabao saba na kufungwa manane. Lakini baada ya Moallin, mabao yanamiminika tu.

Jumla ya mabao 14 yamefungwa kwenye mechi 6 chini ya raia huyo wa Marekani mwenye asili ya Somalia. Katika mechi hizo, Azam FC imeruhusu mabao 5 tu.

Lakini wakati mwingine namba hazitoi picha halisi. Soka ambalo Azam FC inacheza sasa hivi ni kubwa kiasi kwamba hizi namba hazitoshi kuliezea kwa ukamilifu.

Wachezaji wa Azam FC wamebadilika sana, yaani hadi Aggrey Morris sasa hivi anatulizia mpira mgongoni... amini!

Kenneth Muguna, nyota wa Gor Mahia panga pangua kikosi cha Harambee Stars alionekana usajili wa hovyo zaidi chini ya Lwandamina.

Lakini sasa wachambuzi wote Tanzania wanakubaliana kwamba Muguna ni aina ya mchezaji ambaye hajawahi kuwepo nchini katika majukumu ya nafasi yake. Usimguse Tepsie Evans achana kabisa na Rodgers Kola na sijui useme nini kuhusu Ismail Aziz Kader?

Kwa kifupi kila mchezaji wa Azam FC kwa sasa amebadilika na kuonyesha uwezo wa hali ya juu. Watu pekee ambao hawajabadilika ni Idris Ilunga Mbombo na Abdul Haji Omary maarufu kama Hamahama. Hawa watu sijui wana matatizo gani?

Hawana furaha wakiwa na mpira na hawana furaha wakiwa hawana mpira. Hawaonyeshi kabisa kama ni wachezaji wanaostahili kuchezea timu ya Ligi Kuu achana na timu ya kariba ya Azam FC.

Mbombo yaani hata kutuliza mpira kwake ni tatizo. Azam FC inapocheza na Mbombo ni kama inakuwa pungufu kwa mchezaji mmoja. Akipasiwa mpira, hawezi kuulinda... unapotea, halafu hakabi. Sana sana ataanguka chini na kunyoosha mikono kumlalamikia mwamuzi.

Hana mi-kimbio ya kiushambuliaji. Hana uwezo binafsi wa kumtoka mlinzi, lakini zaidi hana kabisa uwezo wa kucheza kwa kuunganisha safu ya ushambuliaji na kiungo (link up play). Wapinzani wala hawapati shida ya kumkaba. Jinsi anavyojiweka tu uwanjani tayari ameshajikabisha.

Mbaya zaidi nafasi za kufunga ambazo anapoteza unaweza unajiuliza, “Mbombo amekutwa na nini?’

Kwa tunaomjua mkongomani huyu tangu akiwa Zambia tunashangaa sana. Mbombo ni straika mabao. Ni straika hasa. Lakini daaah!

Twende kwa Hamahama. Huyu nadhani siyo aina ya wachezaji ambao wanastahili kuwa Azam FC.

Katika maisha yake ya soka akiwa Azam FC ni mara moja tu alikuwa kwenye ubora wa hali juu. Ilikuwa 2019 kwenye mashindano ya Kagame kule Kigali, Rwanda dhidi ya TP Mazembe.

Kile kiwango alichokionyesha siku ile kama angeelendea nacho sasa hivi tungeshamsahau Kapombe kwenye timu ya taifa.

Kocha wake Etienne Ndayi-ragije alimuwekea matumaini ma-kubwa sana kiasi cha kumuweka nje Nicholas

Wadada kwenye mechi mu-himu ya ugenini ya Ko-mbe la Shiri-kisho dhidi ya Triangle ya Zimbabwe.

Nda-yiragije akitafuta matokeo ya kupindua meza, akamuamini Hamahama ugenini. Unaweza kuona ni namna gani alimuona kama kesho ya Azam FC. Lakini hakufanya kitu mbele ya Ndayiragije, na makocha wengine wote waliokuja baada ya hapo.

Aristica Cioaba alipendekeza aondolewe kwa mkopo na kumtaka Salum Kimenya wa Tanzania Prisons, lakini ikashin dikana. Hamahama akabaki akipewa muda wa kuboresha uwezo wake.

Alipokuja George Lwandamina, akamuamini tangu siku ya kwanza na kumuweka benchi Wadada. Lakini muda mchache baadaye akabaini kwamba yaliyomo aliyodhani kayaona kwake kumbe hayamo. Maisha yanaendelea hivyo hivyo kwa Master Lecturer.

Wa-chezaji wote wa Azam FC wako dunia nyingine kasoro hawa jamaa wawili.

Nadhani hata Azam FC wenyewe wanaona na tusitegemee kuwaona wachezaji hawa kwenye jezi za Azam msimu ujao. Hawabadiliki, hawaoneshi hamu ya kubadilika.

Yawezekana wasiwe wachezaji wabaya, lakini Azam FC siyo sehemu yao sahihi.

[QUOTE="mhariri, post: 937, member: 122"] [HEADING=1]MZEE WA UPUPU: Azam FC wamebadilika, Mbombo na Hamahama ni shida.[/HEADING] [IMG alt="azam pic"]https://www.mwanaspoti.co.tz/resource/image/3718426/landscape_ratio16x9/1160/652/158bf7fdb2f70f7948f5c9d74c3300e3/tc/azam-pic.jpg[/IMG] TANGU ujio wa kocha mpya wa Azam FC, Abdihamid Moallin, timu hiyo imekuwa tofauti kabisa. Inacheza soka safi, inapata matokeo na inafunga mabao mengi. Kabla ya Moallin, Azam FC ilikuwa haijawahi kupata zaidi ya bao moja kwenye ligi. Ilikuwa imecheza mechi saba, imefunga mabao saba na kufungwa manane. Lakini baada ya Moallin, mabao yanamiminika tu. Jumla ya mabao 14 yamefungwa kwenye mechi 6 chini ya raia huyo wa Marekani mwenye asili ya Somalia. Katika mechi hizo, Azam FC imeruhusu mabao 5 tu. Lakini wakati mwingine namba hazitoi picha halisi. Soka ambalo Azam FC inacheza sasa hivi ni kubwa kiasi kwamba hizi namba hazitoshi kuliezea kwa ukamilifu. Wachezaji wa Azam FC wamebadilika sana, yaani hadi Aggrey Morris sasa hivi anatulizia mpira mgongoni... amini! Kenneth Muguna, nyota wa Gor Mahia panga pangua kikosi cha Harambee Stars alionekana usajili wa hovyo zaidi chini ya Lwandamina. Lakini sasa wachambuzi wote Tanzania wanakubaliana kwamba Muguna ni aina ya mchezaji ambaye hajawahi kuwepo nchini katika majukumu ya nafasi yake. Usimguse Tepsie Evans achana kabisa na Rodgers Kola na sijui useme nini kuhusu Ismail Aziz Kader? Kwa kifupi kila mchezaji wa Azam FC kwa sasa amebadilika na kuonyesha uwezo wa hali ya juu. Watu pekee ambao hawajabadilika ni Idris Ilunga Mbombo na Abdul Haji Omary maarufu kama Hamahama. Hawa watu sijui wana matatizo gani? Hawana furaha wakiwa na mpira na hawana furaha wakiwa hawana mpira. Hawaonyeshi kabisa kama ni wachezaji wanaostahili kuchezea timu ya Ligi Kuu achana na timu ya kariba ya Azam FC. Mbombo yaani hata kutuliza mpira kwake ni tatizo. Azam FC inapocheza na Mbombo ni kama inakuwa pungufu kwa mchezaji mmoja. Akipasiwa mpira, hawezi kuulinda... unapotea, halafu hakabi. Sana sana ataanguka chini na kunyoosha mikono kumlalamikia mwamuzi. Hana mi-kimbio ya kiushambuliaji. Hana uwezo binafsi wa kumtoka mlinzi, lakini zaidi hana kabisa uwezo wa kucheza kwa kuunganisha safu ya ushambuliaji na kiungo (link up play). Wapinzani wala hawapati shida ya kumkaba. Jinsi anavyojiweka tu uwanjani tayari ameshajikabisha. Mbaya zaidi nafasi za kufunga ambazo anapoteza unaweza unajiuliza, “Mbombo amekutwa na nini?’ Kwa tunaomjua mkongomani huyu tangu akiwa Zambia tunashangaa sana. Mbombo ni straika mabao. Ni straika hasa. Lakini daaah! Twende kwa Hamahama. Huyu nadhani siyo aina ya wachezaji ambao wanastahili kuwa Azam FC. Katika maisha yake ya soka akiwa Azam FC ni mara moja tu alikuwa kwenye ubora wa hali juu. Ilikuwa 2019 kwenye mashindano ya Kagame kule Kigali, Rwanda dhidi ya TP Mazembe. Kile kiwango alichokionyesha siku ile kama angeelendea nacho sasa hivi tungeshamsahau Kapombe kwenye timu ya taifa. Kocha wake Etienne Ndayi-ragije alimuwekea matumaini ma-kubwa sana kiasi cha kumuweka nje Nicholas Wadada kwenye mechi mu-himu ya ugenini ya Ko-mbe la Shiri-kisho dhidi ya Triangle ya Zimbabwe. Nda-yiragije akitafuta matokeo ya kupindua meza, akamuamini Hamahama ugenini. Unaweza kuona ni namna gani alimuona kama kesho ya Azam FC. Lakini hakufanya kitu mbele ya Ndayiragije, na makocha wengine wote waliokuja baada ya hapo. Aristica Cioaba alipendekeza aondolewe kwa mkopo na kumtaka Salum Kimenya wa Tanzania Prisons, lakini ikashin dikana. Hamahama akabaki akipewa muda wa kuboresha uwezo wake. Alipokuja George Lwandamina, akamuamini tangu siku ya kwanza na kumuweka benchi Wadada. Lakini muda mchache baadaye akabaini kwamba yaliyomo aliyodhani kayaona kwake kumbe hayamo. Maisha yanaendelea hivyo hivyo kwa Master Lecturer. Wa-chezaji wote wa Azam FC wako dunia nyingine kasoro hawa jamaa wawili. Nadhani hata Azam FC wenyewe wanaona na tusitegemee kuwaona wachezaji hawa kwenye jezi za Azam msimu ujao. Hawabadiliki, hawaoneshi hamu ya kubadilika. Yawezekana wasiwe wachezaji wabaya, lakini Azam FC siyo sehemu yao sahihi. [/QUOTE]
Verification
Kwani 1 + 1 = ni ngapi?
Post reply
Majukwaa
Maskani ya Michezo na Mikeka
Kijiwe cha Ligi Kuu Bongo
AZAM SC
Top
Bottom