Azam Sports Club

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Azam FC Wamtangaza Abdi Hamid Kuwa Kocha Mkuu.​

AZAM-3.jpg

Klabu ya soka ya Azam imemtangaza Abdi Hamid Moallin kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho kwa mkataba wa miaka mitatu akirithi mikoba ya George Lwandamina.
Awali Moallin aliletwa kushika nafasi ya Mkurugenzi wa Ufundi wa Maendeleo ya Soka la Vijana.
“Azam FC ni klabu kubwa, na nililiona hili siku ya kwanza tu nilipofika hapa, nina amini katika klabu hii, nina amini katika uwezo wa klabu hii, klabu hii ina nafasi ya kufanya makubwa,”- Abdihamid Moallin, Kocha Mkuu Azam FC
AZAM-4.jpg

AZAM-1.jpg
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
OFFICIAL: Mlinda mlango wa zamani wa Azam Fc
🇹🇿
Razak Abalora ametambulishwa kuwa golikipa wa Sheriff Tiraspol ya Moldova
🇲🇩
akitokea Asante Kotoko
Sheriff Tiraspol inashiriki kwenye michuano ya UEFA Europa League baada ya kutolewa kwenye Uefa Champions League
Inaweza kuwa picha ya Watu 2, watu wanasimama na ndani
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

ISMAIL AZIZ AONGEZA MWAKA MMOJA AZAM FC.​


MTENDAJI Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ (kushoto) akisaini mkataba na kiungo, Ismail Aziz Kader (kulia) leo Jijini Dar es Salaam.
Kader alijiunga na Azam msimu wa 2020/21 kwa mkataba wa miaka miwili ambao unaisha mwishoni mwa msimu huu na kwa kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja leo sasa ataendelea kupiga kazi Chamazi hadi mwakani.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Azam wazitangazia vita Simba, Yanga.​

prince-dube-azam-2.webp

UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa malengo yao makubwa msimu huu ni kuhakikisha wanashinda michezo mingi kadiri inavyowezekana ili kujiweka kwenye nafasi nzuri katika msimamo na kukata tiketi ya kucheza mashindano ya kimataifa msimu ujao.
Azam ambayo ipo chini ya kocha Abdi Hamid Moallin, kabla ya michezo ya jana ilikuwa kwenye nafasi ya nne na pointi zao 21 walizokusanya kwenye michezo 13.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ ameliambia Championi Jumamosi kuwa: “Tunajua wazi kuwa ligi ya msimu huu ni ngumu na kama klabu kila mtu anajua ni namna gani tulipitia kipindi kigumu mwanzoni mwa msimu huu, lakini kwa sasa tumerekebisha sehemu kubwa ya mapungufu tuliyokuwa nayo.
“Malengo yetu makubwa ni kuhakikisha tunashinda michezo yetu ijayo kadiri itakavyowezekana ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kushiriki mashindano ya Afrika msimu ujao.”
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Dube: Nimerudi Kuwafungia Mabao Azam FC.​

b9c0957f635068c3c0b44a3b1e44d81352f10587.jpg

BAADA ya kupitia kipindi kigumu cha kuandamwa na majeraha, hatimaye straika wa Azam FC, Prince Dube, amesema kuwa kwa sasa yupo fiti, anataka kupambana na kuifungia mabao mengi timu yake.
Dube amesema msimu uliopita alipishana na kiatu cha ufungaji bora kwa sababu alikuwa anaumia mara kwa mara, lakini kwa sasa yupo fiti na anarudi akiwa na nguvu kubwa uwanjani.
Akizungumzia hali yake kiafya na mwenendo wa ligi tangu kuanza kwa msimu huu, Dube alisema kumekuwa na mabadiliko makubwa kwa timu nyingi na ushindani umeongezeka, ila kwa kuwa amepona na kuwa fiti, atafanya kile mashabiki wake wanataka.
“Msimu niliuanza vibaya kutokana na majeraha. Niliumia sana kwa sababu malengo yalikuwa ni kuisaidia timu ila nashukuru nimerejea na nipo tayari kwa hilo,” alisema.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

AZAM FC YAICHAPA NAMUNGO 2-1 RUANGWA​


TIMU ya Azam FC imezinduka na kupata ushindi wa ugenini wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Namungo FC jioni ya leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na Prince Dube Mpumelelo dakika ya 22 na Ismail Aziz Kader dakika ya 35, baada ya Namungo FC kutangulia na bao l Mohammed Issa dakika ya pili.
Azam FC inafikisha pointi 28 baada ya ushindi huo na kurejea nafasi ya tatu, ikiizidi pointi tatu Namungo baada ya wote kucheza mechi 18.