Tafuta
Tafuta vichwa vya habari tu
Kutoka kwa:
Tafuta vichwa vya habari tu
Kutoka kwa:
Nyumbani
Majukwaa
Story Mpya
Tafuta Majukwaa
Story Mpya
Posti Mpya
Posti Mpya za wasifu
Vilivyofanyika
Wanachama
Wanaotembelea kwa sasa
Posti mpya za wasifu
Tafuta Posti za wasifu
Ingia
Jiunge
Tafuta
Tafuta vichwa vya habari tu
Kutoka kwa:
Tafuta vichwa vya habari tu
Kutoka kwa:
Menu
Install the app
Install
Reply to thread
Majukwaa
Maskani ya Michezo na Mikeka
Kijiwe cha Ligi Kuu Bongo
Baada Ya Kipigo Cha 4-1 Jana….Pantev Ashtua Mashabiki Simba Kwa Kauli Hii…’Siwezi….’
JavaScript is disabled. For a better experience, please enable JavaScript in your browser before proceeding.
You are using an out of date browser. It may not display this or other websites correctly.
You should upgrade or use an
alternative browser

Message

KIKOSI cha Simba, jana (Jumapili) kilikuwa kwenye mwendelezo wa maandalizi yake ya kimataifa kwa kucheza mechi ya kirafiki ya pili dhidi ya Al Hilal Omdurman ya Sudan, kwenye Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, ukiwa mchezo wa pili wa kirafiki tangu Dimitar Pantev akabidhiwe timu hiyo.

Mechi hiyo iliyoisha kwa Simba kufungw goli 4-1, ilikuwa sehemu ya programu maalumu ya Pantev, kuelekea mtihani wake wa kwanza dhidi ya Nsingizini Hotspurs ya Eswatini katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wikiendi ijayo.

Katika mechi ya kwanza ya kirafiki kati ya timu hizo ambayo ilipigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1. Ushindi huo ulimpa Pantev taswira ya awali kuhusu uwezo wa kikosi chake na wapi anapaswa kuanzia.

“Siwezi kubadilisha kila kitu kwa wakati mmoja,” amesema Pantev. “Nimeona vijana wanajituma, wanaelewa kile ninachohitaji, niliwaambia nini nahitaji katika mechi hizi, kwangu matokeo sio kitu kwenye mechi za kirafiki ni kuona namna gani kama timu tunacheza, tupo sehemu nzuri.”

Pantev aliongeza kuwa anatambua ugumu wa mechi inayowakabili dhidi ya Nsingizini Hotspurs huku akieleza kuwa lengo la mechi mbili za kirafiki walizocheza ni kujenga maelewano ya kimbinu.

“Tunahitaji kuwa timu inayocheza kwa mpangilio, inayoshambulia kwa hesabu na kulinda kwa umoja. Mechi hizi (za kirafiki) ndizo zinazoniwezesha kuona nani yuko tayari kupigania nembo ya Simba ndani na nje ya uwanja,” amesema kocha huyo ambaye anapendelea kutumia mfumo wa 4-3-3.

Mpaka jana, Pantev alikuwa na asilimia 70 ya kikosi chake kutokana na baadhi ya wachezaji kuwa majukumu ya timu za taifa katika kalenda ya FIFA, lakini alieleza kwamba hali hiyo si kikwazo katika maandalizi yake.

“Ni kawaida wachezaji kuwa majukumu ya kitaifa, lakini ninachokifanya ni kuhakikisha waliopo wanakuwa tayari kimwili na kiakili. Tutakapokuwa wote, itakuwa rahisi kuunganisha mfumo,” amesema.

Baadhi ya wachezaji wa Simba ambao wapo kwenye majukumu ya timu za taifa ni Yakoub Suleiman, Wilson Nangu, Yusuph Kagoma, Seleman Mwalimu na Morice Abraham kwa Taifa Stars ambayo itacheza kesho, Jumanne mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Iran huko Dubai.

Na kwa mujibu wa ratiba, kikosi cha Simba kitaondoka nchini Alhamisi hii (Oktoba 16) kwenda Eswatini kwa ajili ya mechi ya mkondo wa kwanza wa hatua ya pili ya mchujo hivyo huenda kocha huyo asipate muda wa kutosha kufanya maandalizi na wachezaji hao hivyo itambidi kuwa na mpango mbadala.

Simba ilitinga raundi hii ya pili ya mchujo wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuifunga Gaborone United ya Botswana katika hatua ya awali kwa jumla ya mabao 2-1 huku Nsingizini Hotspurs ikipita kwa matuta (4-2) baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba Bhora ya Zimbabwe.

Mshindi wa jumla kati ya Simba na Nsingizini Hotspurs atatinga moja kwa moja katika hatua ya makundi.

Kuhusu nguvu ya mpinzani ambaye wanaenda kukabiliana naye, Pantev alibainisha kwamba; “Ni kawaida kufanya tathimini ya mapinzani wako lakini tumeelekeza nguvu zetu katika maandalizi yetu, tunajua kuwa tunaenda kukutana na timu ngumu kufungika.”

Katika mechi tatu ambazo Nsingizini Hotspurs imecheza msimu huu katika mashindano yote, imeruhusu bao moja tu na ilikuwa katika mechi ya kwanza ya kimataifa dhidi ya Simba Bhora wakiwa ugenini kabla ya kujibu mapigo na kupindua meza kwenye mechi ya marudiano nyumbani.

Kwa upande wa mashindano ya ndani, Nsingizini Hotspurs imecheza mechi moja na kuibuka na ushindi wa bao 1-0. Kwa takwimu zao za msimu uliopita, timu hiyo ngeni kwenye michuano ya kimataifa, ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Eswatini kufuatia kushinda mechi 19, sare tatu na kupoteza nne.

Walikuwa na wastani wa kufunga karibu mabao mawili (1.6) kwenye kila mechi.

Walifunga jumla ya mabao 44 kwenye mechi 26 za Ligi, wameruhusu mabao 14 sawa na wastani wa kuruhusu bao moja kwenye kila baada ya mechi mbili. Ndio timu iliyoruhusu mabao machache zaidi kwenye ligi yao.

[QUOTE="Hammy36, post: 16554, member: 617"] KIKOSI cha Simba, jana (Jumapili) kilikuwa kwenye mwendelezo wa maandalizi yake ya kimataifa kwa kucheza mechi ya kirafiki ya pili dhidi ya Al Hilal Omdurman ya Sudan, kwenye Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, ukiwa mchezo wa pili wa kirafiki tangu Dimitar Pantev akabidhiwe timu hiyo. Mechi hiyo iliyoisha kwa Simba kufungw goli 4-1, ilikuwa sehemu ya programu maalumu ya Pantev, kuelekea mtihani wake wa kwanza dhidi ya Nsingizini Hotspurs ya Eswatini katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wikiendi ijayo. Katika mechi ya kwanza ya kirafiki kati ya timu hizo ambayo ilipigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1. Ushindi huo ulimpa Pantev taswira ya awali kuhusu uwezo wa kikosi chake na wapi anapaswa kuanzia. “Siwezi kubadilisha kila kitu kwa wakati mmoja,” amesema Pantev. “Nimeona vijana wanajituma, wanaelewa kile ninachohitaji, niliwaambia nini nahitaji katika mechi hizi, kwangu matokeo sio kitu kwenye mechi za kirafiki ni kuona namna gani kama timu tunacheza, tupo sehemu nzuri.” Pantev aliongeza kuwa anatambua ugumu wa mechi inayowakabili dhidi ya Nsingizini Hotspurs huku akieleza kuwa lengo la mechi mbili za kirafiki walizocheza ni kujenga maelewano ya kimbinu. “Tunahitaji kuwa timu inayocheza kwa mpangilio, inayoshambulia kwa hesabu na kulinda kwa umoja. Mechi hizi (za kirafiki) ndizo zinazoniwezesha kuona nani yuko tayari kupigania nembo ya Simba ndani na nje ya uwanja,” amesema kocha huyo ambaye anapendelea kutumia mfumo wa 4-3-3. Mpaka jana, Pantev alikuwa na asilimia 70 ya kikosi chake kutokana na baadhi ya wachezaji kuwa majukumu ya timu za taifa katika kalenda ya FIFA, lakini alieleza kwamba hali hiyo si kikwazo katika maandalizi yake. “Ni kawaida wachezaji kuwa majukumu ya kitaifa, lakini ninachokifanya ni kuhakikisha waliopo wanakuwa tayari kimwili na kiakili. Tutakapokuwa wote, itakuwa rahisi kuunganisha mfumo,” amesema. Baadhi ya wachezaji wa Simba ambao wapo kwenye majukumu ya timu za taifa ni Yakoub Suleiman, Wilson Nangu, Yusuph Kagoma, Seleman Mwalimu na Morice Abraham kwa Taifa Stars ambayo itacheza kesho, Jumanne mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Iran huko Dubai. Na kwa mujibu wa ratiba, kikosi cha Simba kitaondoka nchini Alhamisi hii (Oktoba 16) kwenda Eswatini kwa ajili ya mechi ya mkondo wa kwanza wa hatua ya pili ya mchujo hivyo huenda kocha huyo asipate muda wa kutosha kufanya maandalizi na wachezaji hao hivyo itambidi kuwa na mpango mbadala. Simba ilitinga raundi hii ya pili ya mchujo wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuifunga Gaborone United ya Botswana katika hatua ya awali kwa jumla ya mabao 2-1 huku Nsingizini Hotspurs ikipita kwa matuta (4-2) baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba Bhora ya Zimbabwe. Mshindi wa jumla kati ya Simba na Nsingizini Hotspurs atatinga moja kwa moja katika hatua ya makundi. Kuhusu nguvu ya mpinzani ambaye wanaenda kukabiliana naye, Pantev alibainisha kwamba; “Ni kawaida kufanya tathimini ya mapinzani wako lakini tumeelekeza nguvu zetu katika maandalizi yetu, tunajua kuwa tunaenda kukutana na timu ngumu kufungika.” Katika mechi tatu ambazo Nsingizini Hotspurs imecheza msimu huu katika mashindano yote, imeruhusu bao moja tu na ilikuwa katika mechi ya kwanza ya kimataifa dhidi ya Simba Bhora wakiwa ugenini kabla ya kujibu mapigo na kupindua meza kwenye mechi ya marudiano nyumbani. Kwa upande wa mashindano ya ndani, Nsingizini Hotspurs imecheza mechi moja na kuibuka na ushindi wa bao 1-0. Kwa takwimu zao za msimu uliopita, timu hiyo ngeni kwenye michuano ya kimataifa, ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Eswatini kufuatia kushinda mechi 19, sare tatu na kupoteza nne. Walikuwa na wastani wa kufunga karibu mabao mawili (1.6) kwenye kila mechi. Walifunga jumla ya mabao 44 kwenye mechi 26 za Ligi, wameruhusu mabao 14 sawa na wastani wa kuruhusu bao moja kwenye kila baada ya mechi mbili. Ndio timu iliyoruhusu mabao machache zaidi kwenye ligi yao. [/QUOTE]
Verification
Kwani 1 + 1 = ni ngapi?
Post reply
Majukwaa
Maskani ya Michezo na Mikeka
Kijiwe cha Ligi Kuu Bongo
Baada Ya Kipigo Cha 4-1 Jana….Pantev Ashtua Mashabiki Simba Kwa Kauli Hii…’Siwezi….’
Top
Bottom