Bodi Ya Simba Sc Mmekiri Mmewauza Wanachama Kwa Miaka 3, Wajibikeni

Mshua

Mgeni
May 27, 2024
34
24
5
Mjumbe wa Bodi ya Simba SC CPA ISSA MASOUD amekiri kwamba shilingi bil. 20 alizoahidi mwekezaji Mohamed Dewij "Mo" hazijawahi kuwekwa popote Bali aligeuza fedha anazotoa Kwa matumizi ya kawaida (kununua mchicha, boxer na kandambili) ndo zihesabike kama uwekezaji wa 20b.

Alichotushangaza zaidi ni pale aliposema Jambo hili wanalijua Kwa miaka 3 Sasa lakini wamekuwa wakitoa Taarifa ya Bodi kwenye mikutano mikuu kuonyesha Mambo ni shwari.

Akaenda mbali zaidi akasema hata usajili wa Wachezaji unafanyika Kwa kificho Bodi haijui na kwamba kuanzia Sasa hawataruhusu hilo maana Hali hiyo imesababisha kusajiliwa Kwa Wachezaji wasio na kiwango Bora cha kuchezea Simba SC.

Hoja yangu ni kwamba, Kwa nini Bodi hii hasa wajumbe waliochaguliwa na wanachama wamekubali Kwa miaka yote 3 kuwauza wanachama waliowachagua na kuungana na wajumbe wa upande wa Mwekezaji kutengeneza Taarifa feki na kuwasomea wanachama kwenye mikutano mikuu?

Kwa hali hii nini faida ya wanachama kuwa na wawakilishi kwenye Bodi kama nao wanaungana na mwekezaji "kudanganya" wanachama? Hata kama lengo ilikuwa kutunza Siri za Bodi, walitegemea kutunza Siri hii Kwa Muda gani?

Kwa hili wajumbe wa Bodi mliochaguliwa na wanachama mmewauza waajiri wenu, Wajibikeni.