Buriani Pelé

kidudumtujr

Mgeni
Dec 14, 2022
50
70
5
Tanzania
Kijana wa ki brazili aliecheza Mpira wa miguu,kandanda,soka,kwa mafanikio makubwa ulimwenguni ambayo mpaka sasa hayaja fikiwa na Mchezaji yoyote.

Gwiji wa Mpira wa Miguu Edson Arantes do Nascimento (Pelé) kama wengi mnavyomtambua aliefanya watu waupende Mpira wa miguu “icon of the Football”Leo tarehe 29 December 2022 amefariki Dunia.

Pele,ambaye ana rekodi ya kufunga magoli 77 katika mechi 92, amekuwa nembo ya mpira wa miguu baada ya kufanikiwa kutwaa taji la kombe la dunia mwaka 1958 akiwa na miaka 17.

Anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji pekee ya kushinda kombe la Dunia mara tatu (3).

Habari kutoka Brazil ambapo alikuwa amelazwa katika hospitali imesema kuwa mfalme huyo wa soka amefariki Dunia leo Alhamisi Disemba 29, 2022 .

Pele ambaye ni moja wa wachezaji Bora kabisa katika historia ya soka aliripotiwa kushindwa kuendelea na matibabu ya chemotherapy katika pambano yake dhidi ya saratani ya tumbo ambayo iligunduliwa mnamo Septemba 2021.

Pumzika kwa amani Gwiji wa Mpira Hakika Familia ya mpira wa Miguu imepata pigo kubwa sana.

Rest in peace Legend.!
 

Attachments

  • 8BAC5D68-03A2-4FDE-AB1B-39AFB9AC111A.jpeg
    8BAC5D68-03A2-4FDE-AB1B-39AFB9AC111A.jpeg
    56.9 KB · Somwa: 0
Last edited:
  • Like
Reactions: UnclRugaRafiki
Nov 26, 2022
28
55
5
1672382554314.jpg
"Siku moja, natumai tunaweza kucheza mpira wa miguu pamoja mawinguni" - Ujumbe wa Pele baada ya Diego Maradona kufariki mwaka wa 2020. Furahieni mchezo wenu huko mbinguni malegendari