CHELSEA YACHOMOLEWA DAKIKA YA MWISHO DARAJANI.

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
1640847585618.png

WENYEJI, Chelsea wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Brighton & Hove Albion usiku wa Jumatano katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
Chelsea ilitangulia kwa bao la Romelu Lukaku dakika ya 28, kabla ya Danny Welbeck kuisawazishia Brighton dakika ya 90 na ushei.
Kwa matokeo hayo, Chelsea inafikisha pointi 42 baada ya kucheza mechi 20, ikisogea nafasi ya pili ikiwa inaizidi pointi moja tu Liverpool ambayo pia ina mchezo mmoja mkononi na timu hizo zitamenyana Jumapili katika mechi ya kuwania nafasi ya pili.
Manchester City ndio inaongoza mbio za ubingwa kwa mbali, ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 20 pia.