CHELSEA YATINGA FAINALI CARABAO CUP

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
1642052473612.png
TIMU ya Chelsea imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup baada ya kuichapa Tottenham Hotspur 1-0 usiku wa Jumatano Uwanja wa Tottenham Jijini London.
Bao pekee la Chelsea limefungwa na Antonio Rudiger dakika ya 18 na kwa matokeo hayo, The Blues inakwenda Fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-0 kufuatia kushinda 2-0 kwenye mchezo wa kwanza na itakutana na mshindi kati ya Arsenal na Liverpool.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

JOTA AIPELEKA LIVERPOOL FAINALI CARABAO CUP.​

AVvXsEgiXP1g3SE9YanQNgzYQE0mYb9rEhtRa6dn2gE3ltZ63ZNvvOcj1xSkvebiONCa2cUz7B_3_t6-xznfST_UsAALWkz408B5tJxKFYl6AIWtC-t70mVY5PIZKFd4u8uGkmNu8sGeBuAfCFz6AixxUf4F426WMQKztP2q9bBkXutga-8sQYqePbxWKxAO=w640-h426

MABAO ya Diogo Jota dakika ya 19 na 77 yameipa Liverpool ushindi wa 2-0 wa dhidi ya wenyeji, Arsenal katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England usiku wa Alhamisi Uwanja wa Emirates Jijini London.
Jota alifunga mabao hayo Nara zote akimalizia kazi nzuri za Trent Alexander-Arnold na kufuatia sare ya 0-0 kwenye mechi ya kwanza Anfield wiki iliyopita, wanakwenda fainali ya Carabao Cup na watakutana na Chelsea Februari 27 Uwanja wa Wembley Jijini London.
Kwa mara nyingine kocha Jurgen Klopp alikuwa mwenye bahati baada ya wapinzani kumaliza pungufu kufuatia Thomas Partey kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 90, yaani dakika 16 tangu aingie kuchukua nafasi ya Emile Smith Rowe.