CHIPUKIZI MWINGINE MTANZANIA ASAJILIWA LIGI YA ISRAEL.

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
MSHAMBULIAJI CHIPUKIZI Mtanzania, Omary Ally Marungu amesajiliwa na klabu ya
Hapoel Kfar Saba FC ya Israel kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Mchezaji huyo aliyeng'ara katika ligi ya vijana ya U20 msimu uliopita akiiwezesha Mtibwa Sugar kutwaa ubingwa amesajiliwa na klabu hiyo ya Daraja la Kwanza Israel, ijulikanayo kama
Liga Leumit baada ya kufuzu majaribio aliyofanya kuanzia mapema mwezi huu.
Anakuwa Mtanzania mwingine kucheza Israel kwa sasa baada ya kiungo Novatus Dismas Miroshi, anayecheza teams: Beitar Tel Aviv Bat Yam FC ya Liga Leumit pia kwa mkopo kutoka 2021 Maccabi Tel Aviv aliyojiunga nayo mwaka jana kutoka Azam FC ya Dar es Salaam.
 

Attachments

  • chipukizi.PNG
    chipukizi.PNG
    598.9 KB · Somwa: 0