Dembele kubaki Barcelona.

1640337911441.png
Winga wa Fc Barcelona Ousmane Dembele amekubali kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa muda wa miaka mitano ijayo
Katika mkataba huo ambao unatarajiwa kutangazwa wiki ijayo, Dembele amekibali kupunguza mshahara wake ili kuruhusu timu hiyo kusajili wachezaji wengine
Ikumbukwe Dembele amekataa maamuzi ya wakala wake ambaye alitaka nyota huyo raia wa Ufaransa akatafute changamoto sehemu nyingine ambazo zilikuwa na ofa nono
Baadhi ya vilabu vilivyokuwa vinahitaji huduma yake ni Manchester United
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿
Newcastle Utd
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿
pamoja na Bayern Munich
🇩🇪
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Licha ya Ousmane Dembele kuendelea kusisitiza kuwa anataka kubaki Fc Barcelona baada ya kukutana na kuzungumza na kocha wake Xavi Hernandez, wakala wa nyota huyo Moussa Sissoko afunguka mazito
"Hatujui itakuwaje, lakini viongozi wa Barca wanampoteza Ousmane wao wenyewe. Tangu mwanzo, tulionyesha kwamba tupo tayari kuzungumza nao kuhusu mkataba mpya bila kuzuizi chochote"
"Wapo kama hawawezi kufanya kazi na watu kama sisi, Labda nafikiri wanaweza kufanya kazi na mawakala ambao ni rafiki wa Barcelona ila Sio kesi yangu, mimi nipo hapa kwaajilj ya kutetea masilahi ya mchezaji wangu."
"Hatupo hapa kwa ajili ya kuchochea mijadala kwenye mitandao ya kijamii, lakini ukweli lazima usemwe. Ndiyo, tunayo matakwa ya kudai, lakini tayari tumeshaonyesha kwamba maamuzi ya mchezaji mwenyewe hayaangalii pesa, vinginevyo asingekuwa hapa. ."
"Kama Barca wangetaka mazungumzo, wangejaribu kuja mezani tuzungumze lakini hadi sasa hakuna mazungumzo yoyote"
Ikumbukwe mkataba wa Ousmane Dembele unamalizika mwishoni mwa msimu huu, tayari vilabu vya Chelsea, Manchester United, Bayern Munich na Newcastle vimeonyesha nia ya kumhitaji.
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1 na nyasi