European Super League mbioni kurejea

Feb 7, 2023
61
36
5
THE EUROPEAN SUPER LEAGUE IS BACK🔥💸📌

Waratibu wa michuano iliyozua taharuki Ulaya “THE EUROPEAN SUPER LEAGUE” wamerejea tena na mpango wao wa michuano hio na wamepanga kufanya mabadiliko ya namna michuano hii itakavyoendeshwa.

Michuano itahusishwa vilabu kuanzia 60 mpaka 80 huku ikichezwa katika madaraja tofauti.

Timu Moja itacheza uwiano wa michezo mpaka 14 kwa Msimu.

KUBWA KULIKO: Wameondoa kipengele cha “Closed Door Tournament” ikiwa na maana kuwa kwa sasa hii michuano itaruhusu timu kuingia na kutoka katika madaraja husika.

Tunafahamu kuwa Timu zilizojihusisha na ESL zimekutana na misukosuko kadha wa kadhaa baada ya KUJIUNGA na mashindano yaliyopingwa na mamlaka nyingi za soka Ulaya.
For Example , Chelsea Take over, Juventus demise, Manchester City Scandals , Liverpool&Manchester United Sale proposals .

Tayari maafisa wa vilabu vya Juventus, Real Madrid na Fc Barcelona wakiongozwa na Rais wa Real Madrid Florentino Perez wameanza Mazungumzo na vilabu takribani 50 ili viweze kujiunga.

Kumbuka lengo Mama la michuano hii ni kuongeza vipato ndani ya vilabu shiriki, huku waanzilishi wa michuano hii wao wanaamini timu zinatumia pesa nyingi kwenye sajili lakini hakuna wanachopata kupitia michuano ya UEFA, hivyo wanaamini kupitia European Super League anaweza akawa mkombozi kwa vilabu vingi barani ulaya.

Je, Mabadiliko Haya ya THE SUPER LEAGUE yatatengeneza urahisi wa kuanzishwa kwa ligi hii ya Wadau?

NB: Kama tumebariki AFRICAN SUPER LEAGUE VIPI TULAANI EUROPEAN SUPER LEAGUE?🤔
20230209_152927.jpg