FIFA

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
FIFA YAIZUIA URUSI KICHEZA NYUMBANI NA...

AVvXsEgl12M0CQ45j1E0ZmACB_VZ2_3u-D95RDsQxoLaXh3twVx1EyrBo-r-PdLPUL3prKpoSZti6pO45OMC0IyTZtOzP21wIj9CrX_8upWyCL56E6_bNuv_aLfY1VgDFRrw7eebxnwQhFP2OOFbdR4cNFYU1Hhns2JEeXjEQvW59BHFV2IO6ljdgnxAE0pR=w640-h468

SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limeitaka Urusi kucheza michezo yake katika Uwanja huru na bila mashabiki ikiwa ni kikwazo baada ya majeshi ya nchi hiyo kuivamia Ukraine na kuishambulia.
Hata hivyo, FIFA imesema timu za Urusi zitashiriki mashindano yote ya bodi hiyo ya soka duniani, ikiwemo Kombe la Dunia baadaye mwaka huu nchini Qatar.
Lakini FIFA imesema katika michezo ya Urusi hakutapeperushwa bendera ya nchi yao wala kuchezwa wimbo wa taifa lao.
FIFA imesema agizo hilo litaanza kwenye michezo ya mchujo wa kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Poland Machi ambao ulipangwa kuchezwa Jijini Moscow.
 
Last edited:

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Klabu ya Schalke 04
πŸ‡©πŸ‡ͺ
imethibitisha kusitisha mkataba wao wa udhamini na kampuni ya GAZPROM ya Russia
πŸ‡·πŸ‡Ί
kutokana na shambulio linaloendelea Ukraine
πŸ‡ΊπŸ‡¦

Ikumbukwe siku chache zilizopita, Schalke waliondoa nembo ya kampuni hiyo mbele ya jezi zao, sasa maamuzi yamefika mbali zaidi hadi kusitisha mkataba
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1 na maandishi yanayosema 'umbro Schalke 04'
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Urusi Yapigwa Chini Kombe la Dunia​

ukraine.jpg

Sasa ni rasmi, Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA imeizuia Urusi kushiriki kombe la dunia mwaka huu huko Qatar hivyo haitaendelea na mechi hata zile za kufuzu.
Urusi ilifanikia kutinga kwenye hatua ya mchujo kufuzu kwa fainali hizo. Timu alizopangwa nazo Urusi katika Kundi lake la kufudhu, ni Jamhuri ya Czech, Poland na Sweden ambazo tayari zimeshatangaza mapema kuwa hazitokuwa tayari kucheza dhidi ya Urusi.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

SIO ZENGWE: Ya Kenya, Zimbabwe yaweza kurudi Tanzania
Kenya PIC

WIKI iliyopita Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) lilitangaza kuzifungia Kenya na Zimbabwe kushiriki katika mchezo huo kimataifa baada ya serikali za nchi hizo kuingilia masuala ya mpira wa miguu.
Nchini Kenya, serikali imeuondoa uongozi wa kuchaguliwa na kuweka kamati ya muda kutokana na tuhuma mbalimbali za ufisadi wa viongozi hao, na umma umekubaliana na kitendo hicho ukisema kwanza hakuna nchi inachopoteza kwa sasa; timu ya taifa haimo mashindanoni hali kadhalika klabu.
Nchini Zimbabwe hali ni kama hiyo. Viongozi wanatuhumiwa kwa ufisadi na unyanyasaji wa kijinsia na hivyo serikali imeona iusafishe mchezo huo. Nilipigiwa simu na redio kadhaa kuomba maoni yangu kuhusu uamuzi huo wa Fifa. Na jibu langu lilikuwa moja tu; hatuna vyombo imara vya soka vinavyoweza kuwawajibisha viongozi wanapokuwa na matatizo au tuhuma za ubadhilifu. Hali hiyo inapotawala, viongozi hujifanyia mambo wapendavyo kwa kuwa chombo pekee kinachoweza kuwawajibisha ni mkutano mkuu ambao idadi ikiwa ndogo kama wa TFF sasa, ni rahisi kucheza nao.
Wale viongozi wa Shirikisho la Soka Kenya (KFF) wamekuwa na tuhuma nyingi na ziliongezeka nguvu baada ya nchi hiyo kurudi kutoka fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) zilizofanyika Misri.
Viongozi walichukua fedha serikalini wakidai za kwenda kuihudumia timu kwa ajili ya malazi na mambo mengine wakati ikiwa Misri. Baadaye zikapatikana taarifa timu ilihudumiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa malazi na mambo mengine.
Tangu wakati huo, si mkutano mkuu wa KFF wala chombo kingine chochote kilichohoji tuhuma hizo na viongozi wakaendelea kula bata.
Ilifikia wakati hadi vyombo vya habari vikaanza kuhoji sababu za Fifa au CAF kutoingilia kati na kuwawajibisha viongozi. Na hata fedha za rushwa za Ahmad Ahmad alizotoa kwa marais wa vyama vya soka walioandika barua ya kumuunga mkono katika uchaguzi hata kabla ya uchaguzi kutangazwa, hazikuhojiwa.
Inapofikia hali kama hiyo, ni lazima serikali iingilie kati na kuchukua hatua kwa kuwa wenye chombo hawaoni tatizo fedha zikiliwa ovyo; isitoshe na wao hula sehemu ya fedha hizo dharimu.
Hali ni tofauti kwa Fifa yenyewe kwa kuwa ina kamati ya maadili ambayo imegawanyika mara mbili. Moja ni kwa ajili ya uchunguzi na nyingine ni kwa ajili ya kuendesha mashtaka.
Ile inayofanya uchunguzi ndiyo iliyobaini kuwa rais wa zamani wa shirikisho hilo, Sepp Blatter aliidhinisha malipo ya dola milioni moja kwa rais wa Chama cha Soka Ulaya (Uefa), Michell Platini katika hali ya utata na ndipo aliposhtakiwa na kufungiwa miaka nane kujihusisha na soka. Tuhuma za Blatter zingewasilishwa kwenye mkutano mkuu wa Fifa, angepeta kilaini.
Sisi tuna Kamati ya Maadili lakini huioni ina nguvu hizo. Kila siku inaadhibu watu walio nje ya uongozi wa TFF. Ina maana hakuna kiongozi mwenye tuhuma mbaya? Hakuna mwamuzi mwenye tuhuma mbaya za rushwa? Hakuna kiongozi wa klabu mwenye tuhuma mbaya za rushwa? Hivi ni kweli ni watu tu wan je ndio wanaokosea kila siku?
Tunahitaji ustaarabu wa hali ya juu kufikia kiwango cha Kamati ya Maadili kuitisha shauri linalomuhusu rais wa TFF na kumuhoji kuhusu tuhuma Fulani za uvunjaji wa maadili. Lakini kwa sasa, tusitegemee kitu kama hicho. Labda tunachoweza kukitegemea ni serikali kuingilia kati kutakapozuka tuhuma za rushwa kama ilivyokuwa enzi za utawala uliopita ambao hatimaye uliishia lupango. Haya yanayotokea Zimbabwe na Kenya yalishatokea sana, lakini utawala wa Leodegar Tenga ukaweka misingi ambayo ilizuia serikali kuingilia kati masuala ya soka. Lakini naona dalili za misingi ile kuondolewa, hali inayoweza kusababisha nchi kurudi huko. Nimeona wazee wa Yanga wameanza kumuomba Rais Samia Suluhu aingilie kati, lakini baadhi wamewakejeli. Maumivu ya kichwa huanza taratibu!
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
OFFICIAL: Beki Yaroslav Rakitskiy (32) raia wa Ukraine
πŸ‡ΊπŸ‡¦
amevunja mkataba wake na klabu ya Zenit St Petersburg ya Russia
πŸ‡·πŸ‡Ί
kutokana na shambulio linaloendelea nchini kwake.
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1