Gharama Za Kutumia Uwanja Wa Uhuru Na Uwanja Wa Benjamin Mkapa

Kijiweni

Administrator
Staff member
Nov 7, 2022
281
396
25
Mwana Kijiweni kama ambavyo leo tumekuja na gharama za viwanja mbalimbali vya soka hapa Tanzania na gharama zake za matumizi sasa utakua ni mmoja ya wale ambao wanatamani kufahamu endapo utataka kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa au Uwanja wa Uhuru gharama zake zikoje? Kutoka kwenye tovuti rasmi ya Wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo katika chapisho lao linalopatikana hapa https://www.michezo.go.tz/pages/national-and-uhuru-stadium-services limeelezea gahrama hizo kama ifuatavyo:

Benjamin Mkapa and Uhuru Stadium Services​

S/NHUDUMAGHARAMA
1.Kukodisha Uwanja wa TaifaTshs. 20,000.000/= au 15% ya mapato ya mlangoni
2.Kukodisha Uwanja wa UhuruTsh.15,000.000/= au 15% ya mapato ya mlangoni
3.Mchezo wa Riadha (Athletics Events)Ths. 3,000,000/=
4.Mazoezi ya Timu (Football Training per session) TaifaTshs. 300,000/=
5.Mazoezi ya timu Uwanja wa Uhuru (Football Training per session)Ths. 200,000/=
6.Matamasha na Maonesho (Exhibitions in open areas Parking area) TaifaThs. 5,000,000/=
7.Sports Bonanza (not in the pitch) Taifa3,000.000/=
8.Sports Bonanza Uwanja wa UhuruThs. 2,000.000/=
9.Ziara za mafunzo,(vikundi/grouos). Mtoto/mwanafunzi /mtu mzima. N.B Gharama hizo zitahusisha ziara kwa viwanja vyote viwili (uhuru na Taifa).Tsh.500/=
Ths.1,000/=
10.Sherehe za Kijamii katika kumbi
(a) VIP Parking (Harusi, Sendoff. N.k.)
(b) Ukumbi Mkubwa Ground Floor
(c)Banquet Hall VIP
(d) Maeneo mengine ya wazi
Ths. 1,000.000/=
Ths. 700,000/=
Tsh. 1,400.000/=
Ths. 1,000.000/=
11.Upigaji picha za mnato na video (harui, Mikanda ya nyimbo n.k)Ths.200,000/=
12.Maegesho ya magari,
VIP Parking nyakati za mchezo
Matamasha na makongamano
Ths. 5,000/=
Ths. 2,000/=
13.Semina, Warsha, Makongamano na Mikutano;
(a) Ukumbi Mkubwa Groung Floor – watu 200
(b) Kumbi ndogo
Tsh. 1,000.000/=
Tsh.200,000/=
Angalizo
1.Gharama za huduma kuanzia namba 1 hadi 13 katika jedwali hapo juu zinahusisha gharama za usafi na ulinzi, pamoja na maandalizi ya Uwanja. (Kiambatanisho No.1)
2.Michezo yote ya kirafiki ya mpira wa miguu itatozwa gharama za awali kiasi cha Tshs. Milioni Tano (5,000,000/=). Iwapo mapato ya Serikali katika mchezo husika yatazidi kiasi tajwa hapo juu yatawasilishwa Wizarani na iwapo mapato yatakuwa chini ama sawa na kiasi tajwa hakutakuwa na madai ya ziada.
3.Michezo yote ya ligi kuu na ile ya CAF na FIFA itaendelea na utaratibu wa kawaida kwa mujibu wa makubalianio kati Serikali na TFF.
4.Gharama za huduma zinaweza kubadilika kulingana na aina ya tukio na ukubwa wake.
 
Last edited:
  • Like
Reactions: edgerchef

swedy

Mpiga Chabo
Sep 10, 2024
1
0
0
Kwa gharama izo kwel mpira wetu unaongozwa na siasa yanga na simba wakijenga viwanja vyao uwanja utakuwa na mapato ya chini sana.