Haji Manara Acha Dharau Na Dhihaka Kwa Ali Kamwe , Yanga SC Imefaidika Nae 'Kibrandi' Kuliko Ulivyokuwepo

Hammy36

Administrator
Jan 17, 2023
54
51
5
Dar Es Salaam
Haji Manara labda nikusaidie Kitaaluma Afisa Habari ndiyo huyo huyo Msemaji acha kutaka Kuwadanganya Watu. Hivi Logically tu Haji Manara kuna tofauti kati ya Information Officer na Communication Manager? Tuliosoma vyema Mass Communication na Kubobea nayo hapa si tu tunakudharau ila pia tunakuona Kichwani zimekupungua.

Tofauti Kuu haya maneno Mawili ya Afisa Habari na Msemaji yanatofautiana tu ni Taasisi gani uliopo ila tunajua ukiwa katika Public Sector utaitwa Afisa Habari na ukiwa katika Private Sector utaitwa Communication Manager na Wengine huitwa Corporate Directors au Chief Communication Officer ila Kimsingi hawa Wote yale Majukumu yao Mama ni yale yale tu.

Wenye Akili Kubwa tunajua kuwa hukuwahi kupatana na Msemaji wa sasa wa Yanga SC Ali Kamwe na hata Kuongea Kwenu ni kwa Kulazimisha na kwa Kinafiki ila Kutwa mnasemana vibaya ( kupigana Majungu ) huku mkiharibiana kwa Tajiri yenu Mkuu GSM na Rais wenu Hersi.

Na kinachokuumiza sasa Haji Manara ni kuona yule Mtu ambaye Kwanza hukumtaka apewe hiyo Nafasi yako si tu kwamba ameiweza vyema hadi Pengo lako Kuzibika ila pia amekuja na Ubunifu wa Kipekee ambao kwa hali ya Sera ya Mpira Biashara ya sasa ndiyo unaotakiwa na Klabu yenye Mafanikio kwa sasa kama ya Watani zangu Yanga SC.

Kwa huku Kurejea Kwako tu ndani ya Yanga SC na kuanza haya Majungu yako naona Vita fulani inakuja mbeleni Ok?
 
  • Like
Reactions: Rhino and Zuu joh

JeffBunKauga

Mpiga Chabo
Jun 5, 2024
5
0
0
Me naona manara angeangalia kingine chafunya akaachan na yang
Afungue Barbershop kama Tawi la Yanga, aendelee kusalia hapo, ili wachezaji na Benchi la ufundi wapate huduma toka Manara Barbeshop & Spa.

Uongozi wa Hersi, jamaa hataki waropokaji na watukanaji. Manara kuna muda anrusha matusi, na si utani wa Jadi. Tusubiri mwafaka wa Club yake.
 

Sir tenge

Mgeni
Jun 5, 2024
11
4
5
Mm naona angeachana na soka tu kwasababu anakipaji kikubwa sana cha mipasho so angejiunga na akina Isha mashauzi aimbe taarab
 

Saidy

Mgeni
Jun 5, 2024
42
10
5
Sielewi mengi kuhusu maswala mazima ya uongozi, ila niseme tu hayo Majungu umeyaona wewe ndg muandishi, na kamwe msipende kukuza vita hadharani 😁 nyie kama viongozi mnatakiwa muwe mstari wa mbele kuboresha uhusiano na sio kuchochea mvurugano. Tambueni kuwa Manara anawafuasi wengi na Ally pia anawafuasi wengi.. kwhy ndg muandishi unaweza kujikuta unagawanya watu na sio kukosanya watu na kuwaweka pamoja.

Sisi kama mashabiki wa Yanga hatujapenda maneno yako ya kutugawanyisha tuanzie kuchagua pakwenda🙏🙏

Acheni uchochezi wa maneno na kukuza vitu ambavyo si vya msingi kisoka.🗣️
 

Mc mikogo

Mpiga Chabo
Jul 8, 2024
2
0
0
104
Manara hajarudishwa Yanga ila kajirudisha mwenyewe tu baada ya kutoka gerezani, jambo lingine analofanya ni kujitekenya mwenyewe na kucheka mwenyewe........

Hayupo tajiri wa ivo anaejua kabisa umefungiwa kwa utovu wa nidhamu halafu akuongeze mshahara, maana yake anatujulisha kuwa JIESIEMU alimtuma amtukane Mista Prezidenti au sio