Hakuna winga bora kwa sasa ndani ya ligi kuu kama Kipre jr

Feb 7, 2023
61
36
5
Azam kwenye dirisha kubwa la usajili walifanya usajili hasa kuanzia golini mpaka mbele, walienda kule Ivory Coast na kumbeba winga fundi kipre Jr.

Jamaa anajua kukaa na mpira mguuni,kuuficha,kukokota,kupiga chenga,ana nguvu, ukitaka acheze kama orthodox au inverted winger anaweza yaan kiufupi ni complete package ya winga anavyotakiwa kuwa.

Ukiangalia kwenye ligi kuu kwa sasa bila kupepesa macho hakuna winga hatari kama kipre Jr,sio Simba wala Yanga wenye winga mwenye kariba ya kipre labda Prime Morisson ambaye na yeye week in, week out.

Kiufupi Azam wamelamba dume,Simba na Yanga wanatamani kuwa na kipre Jr lakini wakikumbuka yupo ndani ya matajiri wa jiji wanaishiwa pozi.

Kongole kwa Scouting team ya Azam,kipre Jr,Isa Ndala na James Akaminko hakika mmepata watu.20230222_225543.jpg