Hapa Dortmund Pale Real Madrid Ni Kivumbi Dimba La Wembley Nani Kuwa Bingwa?

DeviMitupio

Mgeni
May 27, 2024
9
4
5
Dimba la Wembley linalopatikana nchini Uingereza katika jiji la London litawaka moto leo kwani unaenda kupigwa mchezo wa kibabe wa fainali ya ligi ya mabingwa ulaya baina ya klabu ya Real Madrid dhidi ya klabu ya Borussia Dortmund.

Klabu ya Borussia Dortmund wanarudi tena Wembley baada ya miaka 11 kupita kucheza fainali, Kwani mara ya mwisho walicheza fainali katika uwanja huo mwaka 2013 na kuambulia kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Bayern Munich.

Klabu ya Real Madrid watakua wanafukuzia taji lao la 15 kwenye michuano hiyo mikubwa kabisa barani ulaya, Huku klabu ya Borussia Dortmund wao wakiwinda taji lao la pili michuano hiyo baada ya lile waliloshinda mwaka 1997 mbele ya Juventus.

Real Madrid wao wanakwenda kucheza fainali yao ya tisa tangu mwaka 1992, Hku wakiwa wameshinda fainali zao nane zilizopita hivo ni mchezo ambao wanapewa nafasi kubwa zai ya kushinda mchezo huo kutokana na historia kua upande wao kwa kiasi kikubwa.
 

Attachments

  • dad3a2f7-4369-4743-822a-4d2643ae10b8.jpg
    dad3a2f7-4369-4743-822a-4d2643ae10b8.jpg
    256.4 KB · Somwa: 0