Jeshi la Simba lililobeba matumaini ya Wanasimba hadharani

Feb 7, 2023
61
36
5
Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuondoka jioni ya leo kuelekea nchini Uganda kwa ajili ya mchezo wao wa raundi ya tatu dhidi ya Vipers.

Simba kwenye kundi lao mpaka sasa hawana alama yoyote kwenye michezo miwili waliyocheza,wakifungwa yote huku wakiwa hawajafunga goli.

Hivyo matarajio ya wanasimba wengi ni kupata ushindi wao wa kwanza dhidi ya Vipers ili kurudisha matumaini yao ya kufuzu hatua ya robo fainali.

Kikosi cha wachezaji 24 tayari kishatangazwa, na timu inatarajiwa kuondoka leo saa 10 jioni.

Ushindi wa Simba dhidi ya Vipers ugenini utaleta matumaini kwao kuelekea mchezo wa marudiano tarehe 7,March.

Je, bado unaiona nafasi ya Simba kufuzu kwenye kundi C?20230223_124400.jpg