Jezi za Simba bado Pasua kichwa

Feb 7, 2023
61
36
5
Kwa mara nyingine tena Simba kupitia msambazaji wao wa jezi na vifaa mbalimbali vya klabu hiyo Vunja bei wanakwama kuleta jezi kwa wakati.

Wakati wanazindua jezi kwa mara ya kwanza pale Rotana walisema jezi kwa ajili ya mashabiki zitaingia nchini na kuanza kuuzwa rasmi tarehe 15 mwezi huu,lakini leo wanakuja na taarifa kuwa jezi zimekwama Ethiopia.

Unajiuliza hawakufahamu utaratibu wa kusafirisha hizo jezi kwa ndege ukoje?, au hawakufahamu kama kuna mwaka wa Sungura huko China ambapo wachina wote wanasherekea?

Vunjabei anawakosea sana wanasimba katika suala la jezi, ameshindwa kujifunza kutokana na makosa ambayo aliyafanya mwanzoni mwa msimu huu.

Simba ni brand kubwa kwa sasa wahitaji vitu vyao viende kwa wakati kama vilivyopangwa.


20230207_215958.jpg