Jezi za Simba hadharani kuelekea Klabu Bingwa Afrika.

Feb 7, 2023
61
36
5
Klabu ya Simba jioni ya leo wamezindua rasmi jezi zao watakazozitumia kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika, itakayoanza kutimua vumbi rasmi February 11.
Simba wamezindua jezi hizo huku wakiweka wazi kuwa zitaanza kuuzwa february 15 kwa gharama ya 35,000/,huku wachezaji wakianza kuzitumia kwenye mchezo dhidi ya Horoya nchini Guinea.
Kumbuka Simba wamepangwa kundi moja na Raja Casablanca ya Morocco, Horoya na Vipers.
Nini maoni yako mdau juu ya jezi hizi za Simba, unazipa alama ngapi?20230207_215958.jpg