Jua wakati mzuri wa kuingia sokoni

Muwekezaji

Mgeni
Dec 10, 2021
10
3
5
Dar Es Salaam
Ukiingia Uchina kuna watu wengi wanaheshimika sana lakini kuna watu watatu wanaheshimika sana kwenye taifa hilo lenye watu zaidi ya 1.4 bln

Watu hao ni Sun Tzu, Mao Tse Dong (tamka 'Zedong') na Deng Xiapong. Hawa ni watu ambao wamechangia sana ukubwa na uimra wa taifa hilo kutoka barani Asia.

Lakini Sun Tzu licha ya kupendwa sana ndani ya Uchina, pia anapendwa na hata na mataifa ya magharibi kitu ambacho si rahisi sana.

Kwenye kitabu chake cha The Art of War ambapo kwa tafsiri isiyorasmi tunaweza kusema ni 'Sanaa ya Vita' ameeleza mbinu nyingi bora za kushinda vita zinazotumiwa mpaka sasa.

Ikumbukwe tu Tzu aliishi Uchina ya kale hata kabla ya Rais wa kwanza taifa hilo Mao Zedong hajazaliwa. Tzu alikuwa ni Jenerali wa Jeshi, Mwanafalsafa na Mtu wa Mikakati ambaye aliheshimika sana kwa kuwa mwenye mbinu na mikakati bora ya kushinda vita.

Kupitia The Art of War, Sun Tzu anasema "Atakayeshinda vita ni yule anayejua muda gani wa kupigana na muda gani wa kutokupigana" na huo ni ukweli na falsafa hiyo inaweza kutumiwa hata kwenye uwanja wa uwekezaji.

Mwekezaji mzuri ni yule anayejua ni wakati gani aingie sokoni na wakati si wa kuingia sokoni. Unapotaka kutengeneza faida kwenye soko la hisa lazima ujue ni muda gani wa kununua hisa na muda gani si wa kununua hisa.

Siyo kila muda unaweza kununua hisa! Unahitaji kujifunza na kulisoma soko kabla ya kuingia.