Kagera, Simba waahairishwa

mhindi

Mgeni
Nov 29, 2021
17
6
5
Tanzania
PAMBANO la Ligi Kuu Bara kati ya Kagera Sugar na Simba lililokuwa lipigwe leo Saa 10:00 jioni, kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba limeahirishwa kutokana na nyota 16 wa Wekundu wa Msimbazi kugundulika wanaugua mafua makali na kifua.
Sababu za kuhairishwa kwa mchezo huo kupitia taarifa ya Bodi imesema; "Kitabibu wachezaji 16 wa Simba kati ya 22 waliosafiri kwenda Bukoba, wameonekana kuwa na dalili za mafua na kukohoa hali inayochangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa (Seasonal Infulenza), mchezo huo umehairishwa na utapangiwa terehe nyingine kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu.
 
  • Like
Reactions: Amir