Kila la kheri Mnyama

Feb 7, 2023
61
36
5
Simba leo watashuka dimbani kwenye mchezo wao wa pili hatua ya makundi wakiwakaribisha Raja Casablanca kutoka Morocco.

Simba wataingia wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Horoya Ac ugenini,hivyo ataingia akiwa anahitaji alama 3 muhimu kurudisha hali ya kujiamini.

Faida watakayoingia nayo leo ni kucheza mbele ya mashabiki wao 60,000 na wamekuwa na historia nzuri wanapocheza kwenye uwanja wa Mkapa.

Wamekuwa wakiondoka na ushindi dhidi ya mpinzani wao yeyote wanaekabiliana nae kwenye michuano ya CAF.

Mashabiki wa Simba,wadau wa Soka na Serikali kwa ujumla ipo nyuma ya Simba leo kila la kheri Mnyama. 20230218_143556.jpg