Kila la kheri Mnyama

Feb 7, 2023
61
36
5
Simba usiku wa leo watatupa karata yao kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya wenyeji wao Horoya AC huko Guinea.

Mchezo huo unatazamiwa kuwa mkali na ushindani kwani kila timu inahitaji kuanza vizuri kwenye mchezo wake wa kwanza.

Horoya wamekuwa na matokeo mazuri kaenye uwanja wake wa nyumbani, katika mechi tano za mwisho wameshinda mbili, wamesare mbili na kupoteza moja.

Huku Simba wao kwenye mechi zao tano za mwisho ugenini wamefungwa tatu na kushinda mbili.

Hivyo kwa matokeo hayo Simba atahitaji kupambana zaidi ili kuondoka na alama ugenini, hivyo hivyo kwa wapinzani wao.

Nini tutarajie kwenye mchezo huo, tutarajie mchezo wenye kasi, nguvu hasa ukiangalia maumbile ya wachezaji wa Horoya ni makubwa sana, watatumia sana mipira ya juu kama silaha yao.

Hivyo Simba kwenye safu ya ulinzi wanatakiwa kuwa makini sana kwenye kucheza mipira ya juu, wakati huo sitegemei Simba wakishambulia kwa kutumia mipira ya juu nategemea watatumia sana pasi fupi fupi kufika kwenye lango la mpinzani.

Ukiangalia safu ya kiungo ya Simba Chama,Mzamiru na Kanoute wanaweza kufanya hiyo kazi.

So far Kila la Kheri Simba kwenye mchezo wako wa leo, Taifa lipo nyuma yako.20230211_100944.jpg