Kila la kheri Simba, Yanga Kimataifa

Feb 7, 2023
61
36
5
Wawakilishi pekee kutoka Tanzania Simba na Yanga mwishoni mwa juma hili watakuwa uwanjani kupeperusha bendera ya taifa letu.
Simba ambao wameondoka leo majira ya saa 9:35 alfajiri kuelekea Guinea watashuka dimbani siku ya jumamosi majira ya saa 1 usiku kuwakabili Horoya Ac kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika.
Wakati wapinzani wao Yanga walitangulia kuelekea nchini Tunisia nwanzoni mwa wiki hii kuwakabili wapinzani wao Us Monastir kwenye kombe la Shirikisho.
Kwa jinsi timu zote mbili zilivyojiandaa kuanzia kwenye performance yao ndani ya ligi kuu,naamini Yanga na Simba wanaenda kupata matokeo chanya kwenye michezo yao ya Wikiendi hii licha ya kuwa watakuwa ugenini.
Simba wao ni wazoefu kwenye michuano hii ya Afrika hivyo naamini wataendelea pale walipoishia kwenye michuano iliyopita. Lengo kubwa kwao ni kufika hatua ya nusu fainali, mara nyingi wamekuwa wakiishia hatua ya robo fainali kwa jinsi kikosi chao kilivyoundwa na wachezaji wenye uwezo na ujuzi mkubwa kwenye michuano hii naamini wana nafasi ya kutimiza malengo yao.
Wanajangwani wao walishindwa kufika hatua ya makundi kombe la klabu bingwa Afrika, hivyo wameangukia kwenye Shirikisho bado naamini wana nafasi ya kujiuliza walikwama wapi kwenye klabu bingwa na kufanya vizuri huku walipo.
Kwa ubora wa kikosi chao,matokeo wanayoyapata kwenye ligi kuu wakiwa vinara inaenda kuongeza chachu kwao kuelekea michuano hii, naamini Wananchi wanavuka hatua ya makundi na kupenya mpaka robo fainali.
Kila la Kheri Simba na Yanga kufanya kwenu vizuri kimataifa kuna ongeza zaidi thamani ya ligi yetu ambayo kwa sasa ni ligi namba tano kwa ubora Afrika.
 

Attachments

  • 20230209_103144.jpg
    20230209_103144.jpg
    326.9 KB · Somwa: 1
  • 20230209_103057.jpg
    20230209_103057.jpg
    249.9 KB · Somwa: 1
Last edited:
  • Like
Reactions: Azizi and Lukac