Kila la kheri Wananchi, Mwarabu anafungika

Feb 7, 2023
61
36
5
Jioni ya leo Yanga watatupa karata yao ya kwanza kwenye kombe la Shirikisho dhidi ya Us Monastir huko Tunisia.

Kumbukumbu nzuri kwa Yanga ni mara ya mwisho kucheza kwenye ardhi ya Tunisia walifanikiwa kuwafunga Club Africain kwenye hatua ya mtoano.

Hivyo leo wataingia kwa lengo la kutafuta alama tatu au moja, ingawa haitakuwa rahisi kama hawatajiandaa vizuri.

Us Monastir wapo kwenye kiwango bora sana kwa siku za hivi karibuni, katika mechi tano za mwisho walizocheza nyumbani wameshinda mechi nne na kupoteza moja dhidi ya Al Alhly.

Wakati Yanga kwenye mechi tano za ugenini wamepoteza nne na kushinda moja dhidi ya Club Africain,sio namba nzuri lakini wanatakiwq kufuta hilo vichwani mwao na kuingia na malengo mengine hii leo ambayo ni alama muhimu.

Ubora wa kikosi cha Yanga na benchi lao la ufundi chini ya Nabi ni silaha yao kuelekea mchezo wao leo.

20230212_110701.jpg