Kipanya Malapa ndio ni nyota wa zamani wa Yanga na yupo kwenye shughuli zake zakujikimu kimaisha

sharon

Mgeni
Nov 4, 2022
105
89
5
Vichwa vya habari vingi vimekua vikisema "Mchezaji wa zamani wa YANGA SC na Singida United Kipanya Malapa akiwa kwenye shughuli zake za kiuchumi ambapo anauza mishikaki na kachori maeneo ya Buguruni Kona"

Sijaelewa nia yao ila embu tuwe wawazi hapa mlitaka Yanga wafanyaje?

Alikua analipwa mshahara na posho na alisajiliwa kwa pesa na makubaliano

Hiyo kawaida kama ulichezea mshahara unategemea timu waje wakulipe mbona wapo wengi tu wanaoganga maisha hata magoso anauza mihogo ya kukangaa tandale, Mambo ya kawaida sana, nini mchezaji wa Yanga ama Simba wapo wachezaji wa Premier League wana hali kama ya huyu jamaa wamekua madereva

Hii ndio kauli inayosema ukicheza vibaya ujanani utakula kwa uchungu uzeeeni

Maisha ni kuchagua...unaweza kuwa na mshahara mkubwa lkn lifestyle ndo itaamua baadae uishije...vipi kama alikua anapewa mshahara yeye anatumia kula bata? Matokeo yake ndo hayo. Eboue wa Arsenal yuko wap? Ingawa alipata pesa nyingi

Danny amokachi " the bull"alikua analipwa na Chelsea mil 90per wiki,na bado alifilisika Paul Gascoigne gaza alilipwa hela sana leo ni mvuvi,Ronaldinho yukoje? So swala la kiuchumi sio afdavity au guarantee ya kuwa tajiri,huku kitaa tuma mifano ya watu kama hao wengi tu

Kuna wanajeshi wastaafu hawakutunza fedha zao nao wanaishi kwa tabu,na kada nyingine pia.

1677769566843.png