Kiungo wa zamani wa Arsenal, Real Madrid na Ujerumani, Mesut Ozil ametangaza kustaafu soka akiwa na miaka 34.

jamal

Mgeni
Nov 4, 2022
148
90
5
Kiungo wa zamani wa Arsenal, Real Madrid na Ujerumani, Mesut Ozil ametangaza kustaafu soka akiwa na miaka 34.

Ozil aliichezea Arsenal mara 254 na kushinda Vikombe vinne vya FA akiwa na The Gunners.

Ozil pia alichezea Real Madrid mechi 159, akishinda LaLiga na Copa del Rey.

Mesut Ozil aliichezea Ujerumani mechi 92, akifunga mabao 23 na kubeba Kombe la Dunia mwaka 2014.

Ozil ametangaza kustaafu soka kufuatia majeraha ambayo yameathiri uchezaji wake.

Mchezo wake wa mwisho ulikuwa Februari 2 wakati Istanbul Basaksehir ilipochapwa 1-0 na Kayserispor kwenye Ligi Kuu ya Uturuki.

Baada ya miaka 17 ya kuwa mchezaji wa soka wa kulipwa, Ozil ameamua kustaafu soka mara moja.

Ozil alikuwa na safari ya ajabu ya mpira wa miguu ambayo ilikuwa na nyakati na hisia zisizoweza kusahaulika.

Ozil amemaliza kazi yake kwa vilabu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Schalke, Werder Bremen, Real Madrid, Arsenal, Fenerbahce, na Basaksehir.

Ozil anashukuru mashabiki wake wote ambao wamemuonyesha upendo na anatazamia kila kitu kilicho mbele yake na familia yake.
Fr0pOyZXwAIWELQ.jpg