Kocha Simba atoa faili la ubingwa

Mkwavinyika

Administrator
Staff member
Dec 2, 2021
49
9
26
Dar es Salaam
SIMBA imebadilika! Ni kauli ya kocha mkuu wa timu hiyo, Pablo Franco ambaye amesema tangu amekichukua kikosi hicho timu imeimarika, lakini amelia na eneo la ushambuliaji.

Pablo alisema amefanikiwa kulifanya eneo la ulinzi kuwa imara akitolea mfano nyota wake walivyocheza dhini ya Yanga.

pablo-pic.jpg


“Sehemu nyingine ambayo imebadilika kwenye kikosi chetu katika kila mechi tumekuwa na wastani mkubwa wa kutengeneza nafasi za kufunga, lakini bado tunaendelea kuboresha kwenye kumalizia kwani tunatengeneza nafasi nyingi tunatumia chache.

“Simba inayoonekana wakati huu baada ya muda zaidi itaimarika kucheza katika soka la chini la kuvutia, pasi kuanzia nyuma hadi bao kufunga mabao na muda mwingine kushambulia kwa haraka.”

Pablo amekiongoza kikosi cha Simba katika mechi tano za michuano yote hadi sasa tangu apewe mikoba ya kuifundisha akizikabili Ruvu Shooting, Red Arrows (mara mbili), Geita Gold na Yanga.

MECHI YA ASFC

Simba ndio mabingwa wa Kombe la Shirikisho (ASFC) baada ya msimu uliopita kushinda bao 1-0, katika mechi ya fainali dhidi ya watani zao Yanga iliyochezwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.



Wekundu watakuwa na kibarua cha kwanza katika kombe hilo leo saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya JKT Tanzania inayoshiriki Ligi ya Championship.

Simba katika misimu miwili ya mashindano haya 2018 na 2019, waliwahi kuondolewa na timu za madaraja ya chini kwenye mechi za kwanza dhidi ya Green Warriors na Mashujaa.

Beki wa kati JKT Tanzania, Salum Athuman ‘Stopper’ alisema: “Tunacheza na timu kubwa Simba, tutawapa heshima zote, tutacheza kwa nidhamu ila tutaangalia udhaifu wao na kuangalia namna ya kushinda.”