Kombe la FA

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

ARSENAL YATUPWA NJE NA TIMU YA ‘ MCHANGANI’ FA​

1641791855704.png
TIMU ya Championship, Nottingham Forest imerudia ilichokifanya mwaka 2018 katika Kombe la FA kwa kuifunga Arsenal 1-0 usiku wa Jumapili katika mchezo wa Raundi ya Tatu Uwanja wa City Ground.
Bao lililokizamisha kikosi cha Mikel Arteta cha wachezaji makinda limefungwa na Nahodha wa Nottingham, Lewis Grabban dakika ya 82 na hii inakuwa mara ya pili tu kwa Arsenal kutolewa Raundi ya Tatu Kombe la FA ndani ya miaka 25 iliyopita kwa Forest.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

LIVERPOOL YASONGA MBELE KIBABE KOMBE LA FA ENGLAND.​

1641792313902.png
TIMU ya Liverpool imetoka nyuma na kushinda 4-1 dhidi ya Shrewsbury Town katika mchezo wa Raundi ya Tatu Kombe la FA England usiku wa Jumapili Uwanja wa Anfield.
Daniel Udoh alianza kuwafungia wageni dakika ya 27, kabla ya Liverpool ‘kuliamsha dude’ kwa mabao ya Kaide Gordon dakika ya 34, Fabinho mawili, moja kwa penalti dakika ya 44 na lingine dakika ya 90 na ushei na Roberto Firmino dakika ya 78.
Mechi nyingine, Tottenham pia imetoka nyuma na kuichapa Morecambe 3-1 wakati West Ham imeitoa Leeds United.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAN UNITED YASONGA MBELE KOMBE LA FA​

1641876932936.png


WENYEJI, Manchester United wamefanikiwa kwenda Raundi ya Nne Kombe la FA England baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Aston Villa bao la kiungo Scott McTominay dakika ya nane akimalizia pasi ya Mbrazil, Frederico Rodrigues de Paula Santos 'Fred' usiku wa jana Uwanja wa Venue Old Trafford Jijini Manchester.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
Matokeo ya droo ya mzunguko wa nne wa kombe la Emirates FA CUP
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿


#EmiratesFACup
1641879083746.png
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

RONALDO AKOSA PENALTI MAN U YATOLEWA FA.​

AVvXsEgQ4H-U3fJj06mAXxQp687mV2qYgHbTrt2VI82hhUtSko_Fbs5eAevTzGfLwC-9XH5F4A1PRFk5oDBO3wRb1FFMj1_iwOJCEO6huwuScr38HJhou4t8jom_BWixMQOOo599F3ENl71qik4EC2GNE0GTPR-kr8TTnA8G9pcNcCOy5zRgKRVi0Pv-_IOO=w640-h430

WENYEJI, Manchester United wametupwa nje ya michuano ya Kombe la FA England baada ya kufungwa kwa penalti 8-7 kufuatia sare ya 1-1 na Middlesbrough usiku wa Ijumaa Uwanja wa Old Trafford.
Nyota Mreno wa Manchester United, Cristiano Ronaldo alikosa penalti dakika ya 20, kabla ya mchezaji wa zamani wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho kuifungia bao kuongoza Manchester United dakika ya 25 na kiungo, Matt Crooks kuisawazishia Middlesbrough dakika ya 64.
Katika mikwaju ya penalti, Anthony Elanga alikosa penalti ya nane iliyokitupa nje kikosi cha kocha Mjerumani, Ralf Rangnick katika Raundi ya Nne Kombe la FA mbele ya timu ya Championship, Middlesbrough.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAN CITY YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA FA​

AVvXsEjq_I5WPw78Utm8puBU1uTxEpYO7bbsvx4UNFEBmPDlUZafHU8RM1PlbzKdG21_awLAOIswMulZlju22sqmAKxDfW16NkE37VqI2IWtUkluCExenF4-C-kApnAS3kpr4ogsr5EMjVB_FAjc-v4CAJoX-afbe96N1TnVFRlRprA39LRoUCFY4ksTgKoD=w640-h432

TIMU ya Manchester City imetinga Robo Fainali ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Peterborough abao ya Man City ya Riyad Mahrez dakika ya 60 na Jack Grealish dakika ya 67 usiku wa Jumanne Uwanja wa Weston Homes mjini Peterborough.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

LUKAKU AIPELEKA CHELSEA ROBO FAINALI FA​

AVvXsEiks3MLrdRTfgYtwBo0WnSbI8B5dwv8v0VgLczvTzNxHixIGoMKZbIBt59gG-Tzk8kT0eU6yIZZuq7Gj1XdQCKBz4FskDmnEv6w33f4IX25lbqlks4xeq30YYUUKAMlsFg0kgCGXUvfJZaOxRGarPsFjWM0nScFbB8r98OiMwvRkjagd3zbcwsgvd0G=w640-h428

TIMU ya Chelsea imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Luton Town usiku wa Jumatano Uwanja wa Kenilworth Road mjini Luton, Bedfordshire.
Mabao ya Chelsea yamefungwa na Saul Niguez dakika ya 27, Timo Werner dakika ya 68 na Romelu Lukaku dakika ya 78, wakati ya Luton Town yamefungwa na Reece Burke dakika ya pili na Harry Cornick dakika ya 40.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MINAMINO AIPELEKA LIVERPOOL ROBO FAINALI FA​

AVvXsEhPppiN9s3gMxIztcApqfLE16MWseCujcuBFZ7HO6rkQDegXBK3jWTdnvdUgt_2d4gDI9iPhVjByVF7015utXWzazsgDPVNVcnHJ5Yd6ruzZEhC_MSSMZn6PgQaZrYZVb9JEdOygyxMQ2ZkQPQJxZOCBRnAc0heHJogEnTrVtySsWOqOQHNuYIGOEFU=w640-h476

WENYEJI, Liverpool wamefanikiwa kutinga Robo Fainali ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Norwich City usiku wa Jumatano Uwanja wa Anfield.
Mabao ya Liverpool yote yamefungwa na Takumi Minamino dakika ya 27 na 39, wakati la Norwich City limefungwa na Lukus Rupp dakika ya 76.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

LIVERPOOL YATINGA NUSU FAINALI FA​

8F81A0E4-DB4B-45C9-B42A-4D543E498380.jpeg

LIVERPOOL imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Nottingham Forest Uwanja wa The City Ground Nottingham, Nottinghamshire.
Bao pekee la Liverpool katika mchezo huo limefungwa na mshambuliaji Mreno, Diogo Jota dakika ya 78 na sasa Wekundu hao watakutana na Manchester City mwezi ujao Uwanja wa Wembley Jijini London.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

CHELSEA YAIFUATA LIVERPOOL FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND​


TIMU ya Chelsea imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Crystal Palace Jumapili Uwanja wa Wembley Jijini London.
Katika mchezo huo mkali wa Nusu Fainali, mabao ya The Blues yamefungwa na Ruben Loftus-Cheek dakika ya 65 na Mason Mount dakika ya 76.
Sasa Chelsea watakutana na Liverpool katika Fainali Mei 14, yakiwa ni marudio ya Fainali ya Carabao Cup ambayo Liverpool ilishinda kwa penalti 11-10 baada ya sare ya 0-0 Februari 27 hapo hapo Wembley.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MANE AIPELEKA LIVERPOOL FAUNALI FA, CITY YAFA 3-2 WEMBLEY​


TIMU ya Liverpool imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Manchester City leo Uwanja wa Wembley Jijini London.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na beki Mfaransa, Ibrahima Konaté dakika ya tisa na mshambuliaji Msenegal, Sadio Mane dakika ya 17 na 45, wakati ya Man City yamefungwa na Jack Grealish dakika ya 47 na Bernardo Silva dakika ya 12 ya muda wa fidia baada ya kutimia dakika 90 za kawaida.
Sasa Liverpool itamenyana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili Jumapili baina ya Chelsea Crystal Palace katika Fainali itakayofanyika Mei 14 hapo hapo Wembley.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

LIVERPOOL YATWAA KOMBE LA FA BAADA YA MIAKA 16​



TIMU ya Liverpool imefanikiwa kutwaa Kombe la FA England baada ya miaka 16 kufuatia ushindi wa penalti 6-5 timu hizo zikitoka kumaliza dakika 120 bila kufungana Uwanja wa Wembley Jijini London.
Waliofunga penalti za Liverpool ni James Milner, Thiago Alcântara, Roberto Firmino, Trent Alexander-Arnold, Diogo Jota na Konstantinos Tsimikas, huku Sadio Mane pekee akikosa mkwaju wake ukiokolewa na kipa Msenegal mwenzake, Édouard Mendy.
Upande wa Chelsea waliofunga ni Marcos Alonso, Reece James, Ross Barkley, Jorginho na Hakim Ziyech huku César Azpilicueta na Mason Mount wakikosa.