Kumbe basi la Simba limeuzwa

Kriss

Mgeni
Nov 4, 2022
102
138
5
MWENYEKITI wa Klabu ya Simba ambaye anamaliza muda wake na anaomba kura za kuendele kugombea nafasi hiyo kwenye uchaguzi unaotarajia kufanyika Januari 29, Murtaza Mangungu amekiri kuwa basi la timu hiyo limeuzwa na sio bovu kana inavyoelezwa.

Simba ambayo ni muda sasa basi lao limekuwa halionekani huku wakitumia basi dogo ‘Coaster’ na taarifa ya awali ikithibitisha kuwa basi ni bovu sasa imethibitika kwa limeuzwa.

“Nashushiwa lawama ambazo sio zangu basi la Simba limeuzwa mimi nikiwa sipo kwenye uongozi sikuwa Mjumbe wa Bodi wala Mwenyekiti wa timu hii kama nilivyo sasa,” alisema na kuongeza;

“Lakini baada ya kuingia kwenye uongozi hili suala lilipelekwa kwenye Bodi ya klabu na wajumbe tumelifuatilia na kubaini kuwa limeuzwa kwa kufuata utaratibu,”


1674205777639.png