Kushinda mataji ni tabia

Feb 7, 2023
61
36
5
Ni miaka sita tangu United washinde taji lao la mwisho,lilikuwa Europa league chini ya Mourinho baada ya hapo wamekaa kwa kipindi chote bila taji.

Leo katika dimba la Wembley chini ya kocha Eric Ten Hag wametwaa taji lao la kwanza dhidi ya Newcastle.

Kutwaa taji hili inakuwa hamasa kwa mashabiki,wachezaji na benchi la ufundi kuhitaji kushinda zaidi mataji mengine. Kumbuka United bado wapo kwenye Europa league, FA CUP na bado wanagombea ubingwa wa EPL.

Lakini pia kitu kizuri zaidi kwa United ni juu ya performance yao wanayoonyesha wachezaji wanaonekana kujituma zaidi kutimiza majukumu yao,kwao nawaona bado wana nafasi ya kutwaa taji lingine msimu huu.

ETH AT THE WHEEL 20230226_224422.jpg
 
  • Like
Reactions: McRay