Kuteleza sio kuanguka, Simba bado wana nafasi ya kufanya vizuri

Feb 7, 2023
61
36
5
Matokeo ya jana waliyopata Simba ugenini sio mazuri, hivyo wanahitaji kuyasahau haraka iwezekanavyo kuelekea mchezo wao unaofuata dhidi ya Raja Casablanca.

Jana Simba hawakucheza vizuri sana, ingawa walitengeneza baadhi ya nafasi lakini wakashindwa kuzitumia kupata magoli.

Bocco jana hakuwa kwenye kiwango bora kabisa alipoteza nafasi ambazo zingeisaidia Simba kuondoka na alama moja au tatu, lakini anatakiwa asahau hilo haraka kabisa iwe kama sehemu ya mchezo.

Mara zote soka la Afrika, mwenyeji anakuwa na nafasi kubwa ya kuondoka na ushindi bila kujali anacheza na mpinzani mwenye kiwango gani, kwahiyo kilochotokea kwa Simba jana ni sehemu ya kasumba ya soka la Afrika.

Kocha Robetinho jana alianza na 4-3-3, chaguo ambalo lilifanya timu isicheze vizuri Chama kutokea pembeni kuna ubora unaukosa kutoka kwake.

So far, Raja Casablanca watakuwa na kesi ya kujibu kwa Mkapa ukizingatia kwa Mkapa ni uwanja ambao Simba amekuwa na historia nzuri. 20230212_111815.jpg