Kwa Matokeo ya Man United, bado unawaona kwenye mbio za Ubingwa?

Feb 7, 2023
61
36
5
Manchester United usiku wa kuamkia leo waliwakaribisha Leeds United kwenye dimba lao la Old Trafford, mchezo wa ligi kuu Uingereza.
Katika mchezo huo hakuna aliyeamini kama Manchester United watatoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Leeds kwa jinsi mashetani hao wekundu walivyokuwa kwenye kiwango bora.
Lakini Leeds hawakujali hilo waliingia kwenye mchezo huo kwa kasi kubwa na wakafanikiwa kutawala sehemu kubwa ya mchezo kipindi cha kwanza na kufanikiwa kuongoza kwa mabao mawili.
Kipindi cha pili Man United wakafanikiwa kusawazisha na kufanya mechi kumaliza kwa sare.
Kwa matokeo hayo sasa,United wanafikisha alama 43 katika michezo 22 wakiwa nyuma ya City wenye alama 45 na michezo 21 wakati Arsenal akiwa kinara kwa alama 50 katika michezo 20 aliyocheza mpaka sasa.
Je,kwa msimamo huo bado unaiona nafasi ya Man United kuwania ubingwa wa ligi kuu ambao mara ya miwsho kushinda ni miaka 10 nyuma?.20230209_145440.jpg