Kwa sasa ni Muhimu Fei toto kucheza kwa afya ya soka lake na taifa kwa ujumla

Feb 7, 2023
61
36
5
Ni takribani miezi mitatu sasa tangu kiungo Feisal Salum kuandika barua ya kuvunja mkataba dhidi ya muajiri wake Yanga,kwa kile kinachodaiwa ni maslahi madogo anayopata.

Feisal alifanya hivyo kwa kuona kile anachofanya uwanjani na anachopata ni vitu viwili tofauti,hivyo aliamua kuvunja mkataba kwa mihemko bila kufuata kanuni na taratibu za kufanya hivyo.

Kwa alichokifanya Fei toto au aliyemshauri Fei kufanya hivyo naamini wanajutia kwa sasa juu ya walichokifanya,na maamuzi yashatolewa na TFF kuwa Feisal Salum bado mchezaji halali wa Yanga.

Kwa mantiki hiyo Fei anatakiwa kurejea ndani ya timu hiyo,lakini kwa hali ilivyo Feisal na familia yake wamegoma kurejea ndani ya klabu hiyo.

Feisal Salum ana hatarisha kiwango chake kwa kutocheza kwa muda mrefu sasa,lakini pia Taifa linaweza kukosa hazina ya kiwango chake.

Kitu pekee kinachotakiwa kufanyika kwa sasa ni Feisal na Yanga wamalizane kwa kufuata taratibu zilivyo,kama wanataka kuvunja mkataba wao ambao unamalizika mwaka 2024 basi litakuwa jambo jema au kama kuna timu inamuhitaji Feisal basi wanatakiwa kukaa chini na Yanga ili wamalizane vizuri.

Hii italeta afya kwenye Maendeleo ya Feisal na soka letu kwa ujumla,mpaka sasa Feisal anaonekana ameshindwa kwenye hii kesi. 20230303_091114.jpg