Tafuta
Tafuta vichwa vya habari tu
Kutoka kwa:
Tafuta vichwa vya habari tu
Kutoka kwa:
Nyumbani
Majukwaa
Story Mpya
Tafuta Majukwaa
Story Mpya
Posti Mpya
Posti Mpya za wasifu
Vilivyofanyika
Wanachama
Wanaotembelea kwa sasa
Posti mpya za wasifu
Tafuta Posti za wasifu
Ingia
Jiunge
Tafuta
Tafuta vichwa vya habari tu
Kutoka kwa:
Tafuta vichwa vya habari tu
Kutoka kwa:
Menu
Install the app
Install
Reply to thread
Majukwaa
Maskani ya Michezo na Mikeka
Kijiwe cha Ligi Kuu Bongo
Ligi Kuu Thread
JavaScript is disabled. For a better experience, please enable JavaScript in your browser before proceeding.
You are using an out of date browser. It may not display this or other websites correctly.
You should upgrade or use an
alternative browser

Message

MZEE WA UPUPU: Wamekumbwa na nini?

Ligi Kuu Bara iko katika mzunguko wa pili na timu zote zimeshacheza mechi 17. Ukweli mchungu kuhusu hilo ni kwamba hadi sasa wafungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, wana hali mbaya sana.

Ni wachezaji sita tu msimu uliopita ambao walifikisha tarakimu mbili kwenye idadi ya mabao yao, yaani walifunga mabao zaidi ya tisa...kuanzia kumi.

Wachezaji hao ni John Bocco (Simba) - mabao 16, Chris Mugalu (Simba) - mabao 15, Prince Dube (Azam) - mabao 14,

Maddie Kagere (Simba) - mabao 13, Idd Nado (Azam) - mabao 10 na Danny Lyanga (JKT TZ) - mabao 10,

Hao ndio wachezaji pekee msimu uliopita waliofunga mabao ya idadi ya tarakimu mbili na walitarajiwa msimu huu kuanzia walipoishia, lakini wapi.

JOHN BOCCO

Mfungaji bora mara mbili wa Ligi Kuu Bara 2011/12 na 2020/21. Tanzania inamtambua Bocco kama mmoja washambuliaji hatari katika kizazi chake.

Tangu ajiunge na Simba katika msimu wa 2017/18 akitokea Azam FC, Bocco amekuwa akifunga mabao zaidi ya 10 kila msimu, kasoro msimu mmoja tu - 2019/20 ambao alifunga mabao tisa.

Kwa ujumla huu ni msimu wa 14 kwake tangu aanze kucheza ligi kuu 2008/09 na ameshafunga mabao 142. Msimu wake wa kwanza, 2008/09, alifunga bao moja tu, na hii ni kutokana na uchanga wake wakati huo na wapinzani wake wa namba kikosini.

Yahya Tumbo, Nsa Job na Philip Alando walikuwa wachezaji wakubwa waliomzidi kila kitu. Hakupata namba mbele yao. Kukosa namba kukamfanya aonekane mzigo kikosini na alipendekezwa kukatwa mwisho wa msimu na mmoja wa makocha wake wazawa, lakini Mungu akamsimamia.

Msimu mwingine mgumu kwake ulikuwa 2014/15 ambao alifunga mabao matatu tu. Hata hivyo alitumia sehemu kubwa ya msimu huo akiuguza majeraha aliyoyapata Rwanda kwenye Kombe la Kagame alikoumizwa na Pascal Wawa (huyuhuyu) wa El Merreikh kwenye robo fainali.

Ukiacha misimu hiyo ambayo sababu zake zinaeleweka, Bocco hakuwahi kuwa na msimu mbaya kama huu. Hadi ligi inafika mchezo wa 17 hajafunga hata bao moja na amecheza asilimia kubwa ya mechi hizo.

CHRIS MUGALU

Alitokea Lusaka Power Dynamos ya Zambia akitajwa kama mmoja wa washambuliaji hatari wanapokuwa timamu kimwili. Na kweli, huko kuwa timamu kimwili hakukutajwa burebure au kwa bahati mbaya.

Maisha ya Mugalu ndani ya Simba yamekuwa ya kuumia umia sana. Sehemu kubwa ya maisha yake klabuni hapo ameitumia akiwa hospitali kutokana na majeraha. Mabao yake 15 msimu uliopita yalikaribia kumpa kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora kama siyo penalti ya dakika za mwisho iliyopigwa na kufungwa na Bocco.

Hadi sasa Mugalu hajafunga hata bao moja kutokana na kukosekana uwanjani kwa muda mrefu.

PRINCE DUBE

Alikuwa na msimu mzuri 2020/21. Alifunga mabao ya kuunganisha kwenye mstari na alifunga mabao ya mbali. Alifunga kwa mguu wa kulia na akafunga kwa mguu wa kushoto. Alifunga kwa kichwa na alifunga tumbo. Alifunga kwelikweli.

Lakini, majeraha yaliyoanzia kwenye mchezo dhidi ya KMC pale Chamazi yalikuja kumgharimu baadaye na kumuweka nje msimu wote uliobaki na mwanzoni mwa msimu huu.

Tukiwa kwenye mechi za 17, Dube hajafunga hata bao moja la ligi.,Majeraha yake na mbinu sahihi za timu pinzani kumdhibiti vimempa wakati mgumu na kumfanya hadi sasa aonekane mchezaji wa kawaida.

Ujio wa Mzambia Rodgers Kola pia ni tatizo kwake kwani kocha Abdihamid Moallin anamtumia zaidi Mzambia kama mshambuliaji kinara huku Dube akitumika zaidi kama winga au msaidizi wa Kola.

MEDDIE KAGERE

Mfungaji bora katika misimu miwili mfululizo ya kabla ya msimu huu; 2018/19 na 2019/20. Msimu uliopita hakuonekana sana uwanjani kutokana misimamo ya kocha wake raia wa Ubelgiji, Van de Broeck.

Lakini, hata hivyo alijitutumua na angalau kufikisha mabao 13. Msimu huu ameshafunga mabao matano na kumfanya angalau kuwa na afadhali mbele ya wenzake. Lakini, hata hivyo ukiyachambua mabao yenyewe utaona kwamba naye ni walewale tu.

Mabao matatu kati ya hayo matano ameyafunga kwa penalti zenye utata. Mabao mengine mawili amefunga dhidi ya wapinzani walipopungua baada ya mchezaji mmoja kuony eshwa kadi nyek undu. Kwa hiyo hata yeye haone kani kama ni hatari kiasi hicho.

IDD NADO

M moja wa wachezaji waliokuwa na kiwango bora msimu uliopita. Alihusika katika mabao 18 ya Azam FC; akifunga mabao 10 na kutoa pasi nane zilizozaa mabao. Msimu huu hadi sasa amefunga bao moja tu.

Na hii inatokana na majeraha makubwa aliyoyapata Novemba 30, 2021 ambayo yanamuweka nje kwa miezi tisa. Lakini hata kabla hajaumia Nado alikuwa tayari ameshacheza mechi saba na kufunga bao moja pekee, ikiwa ni dalili za kuanza vibaya msimu.

DANNY LYANGA

Katika vinara wa mabao wa msimu uliopita, Danny Lyanga ndiye mchezaji anaichezea timu ambayo hakuwa nayo msimu uliopita. Alifunga mabao 10 akiwa na JKT Tanzania na sasa yuko Geita Gold ambayo ameshaifungia mabao manne.

Angalau yeye unaweza kumpa faida ya mashaka kwamba amefanya vizuri hadi sasa. Amefunga mabao safi kabisa bila utata wala tata. Ukizingatia yuko katika timu mpya na ambayo ni ngeni kwenye ligi unaweza kumpa heshima kwamba angalau kafanya vizuri.

SIMBA SC

Unapozungumzia vinara wa mabao siyo tu wachezaji, lakini hata timu pia zinahusika. Kwa misimu yote minne ambayo Simba SC wamekuwa mabingwa wa Tanzania wao ndio walikuwa vinara wa kupachika mabao. Lakini, msimu huu tukiwa katika mchezo wa 17 Simba hawajafikisha hata mabao 20.

Msimu uliopita katika mechi 17 walikuwa wameshafikisha mabao 40. Kuondoka kwa mashine zao mbili, Luis Miquisone na Clatous Chama kulipunguza uhatari katika safu ya ushambuliaji. Ukichanganya na tatizo lao kuu msimu huu la kukosa penalti, Simba wamekuwa wa kawaida sana mbele ya lango la mpinzani.

HITIMISHO

Bado kuna michezo 13 mbele na chochote kinaweza kutokea maana mpira wa miguu una maajabu yake. Lakini, hadi sasa kitu pekee ambacho unaweza kusema ni kwamba huu sio msimu bora kabisa kwa vinara wa mabao wa msimu uliopita.

[QUOTE="mhariri, post: 1216, member: 122"] [HEADING=1]MZEE WA UPUPU: Wamekumbwa na nini?[/HEADING] [IMG alt="dube pic"]https://www.mwanaspoti.co.tz/resource/image/3741936/landscape_ratio16x9/1160/652/7d1432e4b8f6ccc691b310ff19a3b888/Zr/dube-pic.jpg[/IMG] Ligi Kuu Bara iko katika mzunguko wa pili na timu zote zimeshacheza mechi 17. Ukweli mchungu kuhusu hilo ni kwamba hadi sasa wafungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, wana hali mbaya sana. Ni wachezaji sita tu msimu uliopita ambao walifikisha tarakimu mbili kwenye idadi ya mabao yao, yaani walifunga mabao zaidi ya tisa...kuanzia kumi. Wachezaji hao ni John Bocco (Simba) - mabao 16, Chris Mugalu (Simba) - mabao 15, Prince Dube (Azam) - mabao 14, Maddie Kagere (Simba) - mabao 13, Idd Nado (Azam) - mabao 10 na Danny Lyanga (JKT TZ) - mabao 10, Hao ndio wachezaji pekee msimu uliopita waliofunga mabao ya idadi ya tarakimu mbili na walitarajiwa msimu huu kuanzia walipoishia, lakini wapi. [B]JOHN BOCCO [/B] Mfungaji bora mara mbili wa Ligi Kuu Bara 2011/12 na 2020/21. Tanzania inamtambua Bocco kama mmoja washambuliaji hatari katika kizazi chake. Tangu ajiunge na Simba katika msimu wa 2017/18 akitokea Azam FC, Bocco amekuwa akifunga mabao zaidi ya 10 kila msimu, kasoro msimu mmoja tu - 2019/20 ambao alifunga mabao tisa. Kwa ujumla huu ni msimu wa 14 kwake tangu aanze kucheza ligi kuu 2008/09 na ameshafunga mabao 142. Msimu wake wa kwanza, 2008/09, alifunga bao moja tu, na hii ni kutokana na uchanga wake wakati huo na wapinzani wake wa namba kikosini. Yahya Tumbo, Nsa Job na Philip Alando walikuwa wachezaji wakubwa waliomzidi kila kitu. Hakupata namba mbele yao. Kukosa namba kukamfanya aonekane mzigo kikosini na alipendekezwa kukatwa mwisho wa msimu na mmoja wa makocha wake wazawa, lakini Mungu akamsimamia. Msimu mwingine mgumu kwake ulikuwa 2014/15 ambao alifunga mabao matatu tu. Hata hivyo alitumia sehemu kubwa ya msimu huo akiuguza majeraha aliyoyapata Rwanda kwenye Kombe la Kagame alikoumizwa na Pascal Wawa (huyuhuyu) wa El Merreikh kwenye robo fainali. Ukiacha misimu hiyo ambayo sababu zake zinaeleweka, Bocco hakuwahi kuwa na msimu mbaya kama huu. Hadi ligi inafika mchezo wa 17 hajafunga hata bao moja na amecheza asilimia kubwa ya mechi hizo. [B]CHRIS MUGALU [/B] Alitokea Lusaka Power Dynamos ya Zambia akitajwa kama mmoja wa washambuliaji hatari wanapokuwa timamu kimwili. Na kweli, huko kuwa timamu kimwili hakukutajwa burebure au kwa bahati mbaya. Maisha ya Mugalu ndani ya Simba yamekuwa ya kuumia umia sana. Sehemu kubwa ya maisha yake klabuni hapo ameitumia akiwa hospitali kutokana na majeraha. Mabao yake 15 msimu uliopita yalikaribia kumpa kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora kama siyo penalti ya dakika za mwisho iliyopigwa na kufungwa na Bocco. Hadi sasa Mugalu hajafunga hata bao moja kutokana na kukosekana uwanjani kwa muda mrefu. [B]PRINCE DUBE [/B] Alikuwa na msimu mzuri 2020/21. Alifunga mabao ya kuunganisha kwenye mstari na alifunga mabao ya mbali. Alifunga kwa mguu wa kulia na akafunga kwa mguu wa kushoto. Alifunga kwa kichwa na alifunga tumbo. Alifunga kwelikweli. Lakini, majeraha yaliyoanzia kwenye mchezo dhidi ya KMC pale Chamazi yalikuja kumgharimu baadaye na kumuweka nje msimu wote uliobaki na mwanzoni mwa msimu huu. Tukiwa kwenye mechi za 17, Dube hajafunga hata bao moja la ligi.,Majeraha yake na mbinu sahihi za timu pinzani kumdhibiti vimempa wakati mgumu na kumfanya hadi sasa aonekane mchezaji wa kawaida. Ujio wa Mzambia Rodgers Kola pia ni tatizo kwake kwani kocha Abdihamid Moallin anamtumia zaidi Mzambia kama mshambuliaji kinara huku Dube akitumika zaidi kama winga au msaidizi wa Kola. [B]MEDDIE KAGERE [/B] Mfungaji bora katika misimu miwili mfululizo ya kabla ya msimu huu; 2018/19 na 2019/20. Msimu uliopita hakuonekana sana uwanjani kutokana misimamo ya kocha wake raia wa Ubelgiji, Van de Broeck. Lakini, hata hivyo alijitutumua na angalau kufikisha mabao 13. Msimu huu ameshafunga mabao matano na kumfanya angalau kuwa na afadhali mbele ya wenzake. Lakini, hata hivyo ukiyachambua mabao yenyewe utaona kwamba naye ni walewale tu. Mabao matatu kati ya hayo matano ameyafunga kwa penalti zenye utata. Mabao mengine mawili amefunga dhidi ya wapinzani walipopungua baada ya mchezaji mmoja kuony eshwa kadi nyek undu. Kwa hiyo hata yeye haone kani kama ni hatari kiasi hicho. [B]IDD NADO [/B] M moja wa wachezaji waliokuwa na kiwango bora msimu uliopita. Alihusika katika mabao 18 ya Azam FC; akifunga mabao 10 na kutoa pasi nane zilizozaa mabao. Msimu huu hadi sasa amefunga bao moja tu. Na hii inatokana na majeraha makubwa aliyoyapata Novemba 30, 2021 ambayo yanamuweka nje kwa miezi tisa. Lakini hata kabla hajaumia Nado alikuwa tayari ameshacheza mechi saba na kufunga bao moja pekee, ikiwa ni dalili za kuanza vibaya msimu. [B]DANNY LYANGA [/B] Katika vinara wa mabao wa msimu uliopita, Danny Lyanga ndiye mchezaji anaichezea timu ambayo hakuwa nayo msimu uliopita. Alifunga mabao 10 akiwa na JKT Tanzania na sasa yuko Geita Gold ambayo ameshaifungia mabao manne. Angalau yeye unaweza kumpa faida ya mashaka kwamba amefanya vizuri hadi sasa. Amefunga mabao safi kabisa bila utata wala tata. Ukizingatia yuko katika timu mpya na ambayo ni ngeni kwenye ligi unaweza kumpa heshima kwamba angalau kafanya vizuri. [B]SIMBA SC [/B] Unapozungumzia vinara wa mabao siyo tu wachezaji, lakini hata timu pia zinahusika. Kwa misimu yote minne ambayo Simba SC wamekuwa mabingwa wa Tanzania wao ndio walikuwa vinara wa kupachika mabao. Lakini, msimu huu tukiwa katika mchezo wa 17 Simba hawajafikisha hata mabao 20. Msimu uliopita katika mechi 17 walikuwa wameshafikisha mabao 40. Kuondoka kwa mashine zao mbili, Luis Miquisone na Clatous Chama kulipunguza uhatari katika safu ya ushambuliaji. Ukichanganya na tatizo lao kuu msimu huu la kukosa penalti, Simba wamekuwa wa kawaida sana mbele ya lango la mpinzani. [B]HITIMISHO [/B] Bado kuna michezo 13 mbele na chochote kinaweza kutokea maana mpira wa miguu una maajabu yake. Lakini, hadi sasa kitu pekee ambacho unaweza kusema ni kwamba huu sio msimu bora kabisa kwa vinara wa mabao wa msimu uliopita. [/QUOTE]
Verification
Kwani 1 + 1 = ni ngapi?
Post reply
Majukwaa
Maskani ya Michezo na Mikeka
Kijiwe cha Ligi Kuu Bongo
Ligi Kuu Thread
Top
Bottom