Tafuta
Tafuta vichwa vya habari tu
Kutoka kwa:
Tafuta vichwa vya habari tu
Kutoka kwa:
Nyumbani
Majukwaa
Story Mpya
Tafuta Majukwaa
Story Mpya
Posti Mpya
Posti Mpya za wasifu
Vilivyofanyika
Wanachama
Wanaotembelea kwa sasa
Posti mpya za wasifu
Tafuta Posti za wasifu
Ingia
Jiunge
Tafuta
Tafuta vichwa vya habari tu
Kutoka kwa:
Tafuta vichwa vya habari tu
Kutoka kwa:
Menu
Install the app
Install
Reply to thread
Majukwaa
Maskani ya Michezo na Mikeka
Kijiwe cha Ligi Kuu Bongo
Ligi Kuu Thread
JavaScript is disabled. For a better experience, please enable JavaScript in your browser before proceeding.
You are using an out of date browser. It may not display this or other websites correctly.
You should upgrade or use an
alternative browser

Message

YUPO YUPO SANA

Wakati wadau wengi wakiamini kipa huyo ambaye amethibitisha kuvutiwa na namna makipa chipukizi wanavyopambana kuwa ana muda mfupi wa kuendelea kucheza, mwenyewe amefunguka kuwa bado ataendelea kucheza.

Anasema maisha yake ni soka na hana kazi nyingine zaidi, hivyo katika muda wa kutafuta bado ataendelea kucheza na endapo atafikia kikomo kuitumikia milingoti mitatu mpango wake ni kuwafundisha makipa.

“Unajua watu wananijaji sana kuhusu umri, naomba niwaambie tu bado nina nafasi ya kucheza na wala sina mpango wa kustaafu hivi karibuni. Muda ukifika nitafanya hivyo lakini sio sasa na siwezi kufanya hivyo eti kwa sababu fulani kafanya na kuna wengine nalinganishwa nao lakini niliwakuta,” anasema.

“Watu wanatamani niache kucheza mpira sasa, nikiacha nitakula nini, waniache ni kazi yangu na ndio maana naifanya na timu nyingi tu zinahitaji huduma yangu kama mchezaji.

“Nina malengo mengi sana na ndio maana nimesomea hadi ukocha. Nina leseni B mpaka sasa na pia nina Advanced ya makipa namshukuru sana Mungu kwa hiki kidogo alichonipatia ambacho wengine hawana.”

Lakini, anasema endapo atakuwa kocha timu yake itanyooka kwani hatapenda longolongo kwa kuwa katika maisha yake ya mpira hajawahi kuwa msumbufu hata siku moja.

“Siwezi nikawa kocha au kiongozi halafu mchezaji unipande kichwani, hapana. Kusema kweli nitakuwa mkali sana naumia kuona mchezaji analipwa mshahara na timu fulani halafu kila siku huyohuyo ndiye msumbufu, aisee mimi siwezi kukubali,” anasisitiza.

SIMBA, YANGA, KMC

Kaseja ambaye amecheza kwa mafanikio makubwa Simba na Yanga anakiri kuwa timu hizo zina presha kubwa kutokana na wingi wa mashabiki, hivyo wachezaji hucheza kwa kuzipambania huku wakiwa na hofu kwa mashabiki kutokana na matokeo yatakayopatikana tofauti na KMC japo pia anakiri kucheza kwa presha kutokana na kuwa kiongozi wa timu (nahodha).

“Simba na Yanga kuna presha ya benchi la ufundi, viongozi na mashabiki, lakini hapa KMC mashabiki ni wachache nguvu kubwa ni benchi la ufundi, japo tunaweza tukafungwa na kukalishwa namna ya kujipanga na mechi ijayo, mimi nakuwa na maumivu mara mbili kwani ni nahodha wa timu na nafahamu madhara ya kufungwa kutokana na namna nilivyojengewa nikiwa timu kubwa,” anasema.

“Wingi wa mashabiki katika hizo unaweza kukufanya hata mchezaji ukatoka mchezoni kama hauna malengo na kuamini kile ambacho unatakiwa kukifanya, maana ukikosea kidogo unazomewa, ukifanya vizuri kila mmoja rafiki yako.”

KISA LUNYAMILA ALALA NJAA

Kaseja anasema Edibilly Lunyamila ni staa aliyekuwa akimchanganya akili yake wakati huo akimsikia akitangazwa katika redio kutokana na uwezo wake.

Ilipotokea akamuona uso kwa uso hakuamini macho yake na kuamua kumfukuzia njia nzima na kwa bahati mbaya alishindwa kupata nafasi hiyo.

“Sina kumbukumbu ilikuwa ni mwaka gani Lunyamila alikuwa Kigoma kulikuwa na mashindano yeye hakuniona, ila mimi nilimuona nikaanza kumfuatilia kwa nyuma baada ya mechi kuisha. Sikupata bahati ya kuonana naye na kuzungumza kwani alipanda gari ndogo na kuondoka ndipo nilipoamua kurudi nyumbani.

“Baada ya kukosa bahati hiyo niliamua kurudi nilipotoka na kukuta gari lililokuwa limetubeba wachezaji kwenda kwenye mechi aliyokuwepo Lunyamila siku hiyo limeondoka. Nikaanza kutembea kwa miguu mpaka nyumbani kufika mida ya saa 3 usiku ndio nilifika nyumbani na kukuta nimefungiwa mlango wameshalala. Hapo ili kufunguliwa mpaka uchapwe kwanza fimbo na ndio ulale hakuna kula tena hapo,” anasema na kuongeza alijikuta akiumia nafsi bora hata angeongea na Lunyamila.

MSOMALI AMTOA MCHEZONI

Katika maisha yake ya mpira anasema yapo mambo mengi mengine atakuja kuyaweka wazi pale atakapoacha kucheza mpira, lakini kwa kuwa mpaka sasa anacheza anabaki nayo moyoni.

Licha ya wingi huo wa matukio, anasema kubwa akiwa Mtibwa Sugar walienda kucheza mechi na Kagera Sugar wakafungwa na waliporejea kocha wake Mohamed Msomali alitoa kauli nzito kuwa, “tumepoteza lakini makipa wangu hakuna kitu. Basi niliumizwa sana na hiyo kauli na wakati tunapoteza nilipambana sana lakini bahati haikuwa yetu ila ni jambo ambalo linaniumiza mpaka sasa.”

[QUOTE="Amir, post: 866, member: 20"] [B]YUPO YUPO SANA[/B] Wakati wadau wengi wakiamini kipa huyo ambaye amethibitisha kuvutiwa na namna makipa chipukizi wanavyopambana kuwa ana muda mfupi wa kuendelea kucheza, mwenyewe amefunguka kuwa bado ataendelea kucheza. Anasema maisha yake ni soka na hana kazi nyingine zaidi, hivyo katika muda wa kutafuta bado ataendelea kucheza na endapo atafikia kikomo kuitumikia milingoti mitatu mpango wake ni kuwafundisha makipa. “Unajua watu wananijaji sana kuhusu umri, naomba niwaambie tu bado nina nafasi ya kucheza na wala sina mpango wa kustaafu hivi karibuni. Muda ukifika nitafanya hivyo lakini sio sasa na siwezi kufanya hivyo eti kwa sababu fulani kafanya na kuna wengine nalinganishwa nao lakini niliwakuta,” anasema. “Watu wanatamani niache kucheza mpira sasa, nikiacha nitakula nini, waniache ni kazi yangu na ndio maana naifanya na timu nyingi tu zinahitaji huduma yangu kama mchezaji. “Nina malengo mengi sana na ndio maana nimesomea hadi ukocha. Nina leseni B mpaka sasa na pia nina Advanced ya makipa namshukuru sana Mungu kwa hiki kidogo alichonipatia ambacho wengine hawana.” Lakini, anasema endapo atakuwa kocha timu yake itanyooka kwani hatapenda longolongo kwa kuwa katika maisha yake ya mpira hajawahi kuwa msumbufu hata siku moja. “Siwezi nikawa kocha au kiongozi halafu mchezaji unipande kichwani, hapana. Kusema kweli nitakuwa mkali sana naumia kuona mchezaji analipwa mshahara na timu fulani halafu kila siku huyohuyo ndiye msumbufu, aisee mimi siwezi kukubali,” anasisitiza. [B]SIMBA, YANGA, KMC[/B] Kaseja ambaye amecheza kwa mafanikio makubwa Simba na Yanga anakiri kuwa timu hizo zina presha kubwa kutokana na wingi wa mashabiki, hivyo wachezaji hucheza kwa kuzipambania huku wakiwa na hofu kwa mashabiki kutokana na matokeo yatakayopatikana tofauti na KMC japo pia anakiri kucheza kwa presha kutokana na kuwa kiongozi wa timu (nahodha). “Simba na Yanga kuna presha ya benchi la ufundi, viongozi na mashabiki, lakini hapa KMC mashabiki ni wachache nguvu kubwa ni benchi la ufundi, japo tunaweza tukafungwa na kukalishwa namna ya kujipanga na mechi ijayo, mimi nakuwa na maumivu mara mbili kwani ni nahodha wa timu na nafahamu madhara ya kufungwa kutokana na namna nilivyojengewa nikiwa timu kubwa,” anasema. “Wingi wa mashabiki katika hizo unaweza kukufanya hata mchezaji ukatoka mchezoni kama hauna malengo na kuamini kile ambacho unatakiwa kukifanya, maana ukikosea kidogo unazomewa, ukifanya vizuri kila mmoja rafiki yako.” [B]KISA LUNYAMILA ALALA NJAA[/B] Kaseja anasema Edibilly Lunyamila ni staa aliyekuwa akimchanganya akili yake wakati huo akimsikia akitangazwa katika redio kutokana na uwezo wake. Ilipotokea akamuona uso kwa uso hakuamini macho yake na kuamua kumfukuzia njia nzima na kwa bahati mbaya alishindwa kupata nafasi hiyo. “Sina kumbukumbu ilikuwa ni mwaka gani Lunyamila alikuwa Kigoma kulikuwa na mashindano yeye hakuniona, ila mimi nilimuona nikaanza kumfuatilia kwa nyuma baada ya mechi kuisha. Sikupata bahati ya kuonana naye na kuzungumza kwani alipanda gari ndogo na kuondoka ndipo nilipoamua kurudi nyumbani. “Baada ya kukosa bahati hiyo niliamua kurudi nilipotoka na kukuta gari lililokuwa limetubeba wachezaji kwenda kwenye mechi aliyokuwepo Lunyamila siku hiyo limeondoka. Nikaanza kutembea kwa miguu mpaka nyumbani kufika mida ya saa 3 usiku ndio nilifika nyumbani na kukuta nimefungiwa mlango wameshalala. Hapo ili kufunguliwa mpaka uchapwe kwanza fimbo na ndio ulale hakuna kula tena hapo,” anasema na kuongeza alijikuta akiumia nafsi bora hata angeongea na Lunyamila. [B]MSOMALI AMTOA MCHEZONI[/B] Katika maisha yake ya mpira anasema yapo mambo mengi mengine atakuja kuyaweka wazi pale atakapoacha kucheza mpira, lakini kwa kuwa mpaka sasa anacheza anabaki nayo moyoni. Licha ya wingi huo wa matukio, anasema kubwa akiwa Mtibwa Sugar walienda kucheza mechi na Kagera Sugar wakafungwa na waliporejea kocha wake Mohamed Msomali alitoa kauli nzito kuwa, “tumepoteza lakini makipa wangu hakuna kitu. Basi niliumizwa sana na hiyo kauli na wakati tunapoteza nilipambana sana lakini bahati haikuwa yetu ila ni jambo ambalo linaniumiza mpaka sasa.” [/QUOTE]
Verification
Kwani 1 + 1 = ni ngapi?
Post reply
Majukwaa
Maskani ya Michezo na Mikeka
Kijiwe cha Ligi Kuu Bongo
Ligi Kuu Thread
Top
Bottom