Ligi Kuu ya Tanzania (NBC Premier League) imekua Ligi ya tano (5) Afrika na ya 39 duniani kwa ubora

JohBwax

Mgeni
Nov 4, 2022
84
72
5
Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS) limeitangaza Ligi Kuu ya Tanzania (NBC Premier League) kuwa Ligi ya tano (5) kwa ubora barani Afrika na ya 39 duniani kwa mwaka 2022

Kongole TFF kwa usimamizi wa ligi, hii iwe chachu ya kurekebisha kasoro mbalimbali zinazopigiwa kelele na wadau wa soka/michezo ili tuwe bora zaidi

Sasa wajitahidi Marefa wa michongo kuwaondoe kabisa halafu haki itendeke na mambo ya Simba na Yanga yaishe ili timu zingine ziweze kufanya vizuri

Mkirekebisha upande wa marefa mnaweza kuwa wa tatu au pili, Marefa wa nchi hii ni wa hovyo sana

Pia Ubora wa ligi yetu kwa upande wa Afrika ni nafasi hiyo ya 5 lakini likija suala la mechi za timu ya Taifa katika hizo nchi zilizoorodheshwa kuwafunga ni shughuli nyingine kabisa..! Hili nalo ni tatizo

Mkisimamisha mabahasha ya timu fulani, hii ligi itaendele kuwa bora zaidi.. kuna wakati timu zingine zinacheza vizuri dhidhi ya wapinzani wakubwa, lakini unakuta wanafungwa kwa sababu ya makosa ya makusudi kutoka kwa baadhi ya (wa)mchezaji wenzao.

TFF mkiwa serious kidogo basi ligi yetu inaweza kufika tatu bora shida ni hawa viongozi wetu tunazidi kuona ujanja ujanja mwingi

1675346774630.png