LIONEL MESSI

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
OFFICIAL: Klabu ya PSG imethibitisha kuwa nyota wake Lionel Messi amepata maambukizi ya virusi vya COVID-19
Get well soon Legend.
1641191163305.png
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Messi Atupia PSG Baada Ya Dakika 477.​

72362-16436128395176-1920.webp

HATIMAYE staa wa Paris Saint Germain, Lionel Messi amefanikiwa kufunga bao lake la pili ndani ya Ligue 1 baada ya kupita dakika 477.
Messi alifunga bao lake hilo la pili wakati PSG ikiibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Lille, juzi Jumapili timu yake ikiwa ugenini.
Katika mchezo huo, Messi alifunga bao moja na kutoa asisti moja dhidi ya wapinzani wake Lille.
Staa huyo ambaye ni mshindi wa tuzo za Ballon d’Or mara saba hajawa katika ubora wake hasa kwa kupachika mabao tangu atue katika viunga vya Parc des Princes.
Messi tangu atue Ligue 1 msimu huu wa 2021-22, bao lake la kwanza alifunga Novemba 20, 2021 wakati PSG ikivaana na Nantes na waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo huo ambao alicheza kwa dakika 90.
Mpaka sasa ndani ya Ligue 1 kwa ujumla amehusika katika mabao tisa akifunga mabao mawili na asisti saba akicheza jumla ya dakika 982 sawa na mechi 13 za ligi hiyo kwa msimu huu mpaka sasa.