Liverpool Inahitaji Quality Midfielder..!

ChichaMandi

Mgeni
Dec 15, 2022
65
71
5
Ukiangalia Liverpool Kwa Sasa bila Thiago au Fabinho Inakuwa kama kuku aliyekatwa Kichwa.

Nimeangalia game 3 carabao Dhid ya Manchester City,Epl Dhidi Ya Aston villa na game ya jana Dhidi Ya Leicester City ukiangalia Kwa jicho la Ufundi unagundua mechi zote hizo Liverpool ilizidiwa Eneo la Kiungo Kwa Nini..??

Kuna Viungo Wawili tu Thiago na Fabinho ambao wanaonekana Wana uhai Eneo la Kiungo Mfano ukiangalia Leicester city Jana walianza na Viungo Watano Dhidi Ya Liverpool (Elliot, Henderson na Thiago) Kati ya Hao watatu ni thiago Peke Yake alikuw anaonekana anatimiza majukum yake kikamilifu Alikuwa Anakaba anapiga Pasi anazunguka Eneo Kubwa la uwanja Hiyo ilifanya Leicester City wawe Bora Eneo la Katikati.

Thiago na Fabinho Huwa wanajikuta wanakaba Eneo Kubwa sana la uwanja Hiyo inapelekea wanachoka Mapema angalia goli walilofunga Leicester Henderson anashindwa hata Kufanya faulo ya kiufund mchezaj anapita mbele yake.

Bila mbinu za klopp Liverpool ni weupe Sana Kwa Uwezo Wa mchezaj mmoj mmoj hasa eneo la kiungo kama thiago na Trent wakibanwa kupiga Pasi unaiyona Kabisa Liverpool wanahangaika kuipeleka timu mbele.

Kwa Sasa Liverpool Wanahitaji Mtu Mwingin Kwny eneo la Kiungo ✍🏿
 

Attachments

  • FB_IMG_1672492105338.jpg
    FB_IMG_1672492105338.jpg
    47.9 KB · Somwa: 0