Liverpool Inaonekana kuanza kuamka, baada ya mabadiliko kadhaa kwenye timu

Bangala

Mgeni
Dec 13, 2022
39
24
5
Liverpool Inaonekana kuanza kuamka, baada ya mabadiliko kadhaa kwenye timu.

Ingizo la kijana mdogo Stefan Bajcetic limerejesha nguvu iliyopotea kwenye eneo la kati la Liverpool.

Cody Gakpo anaonekana kuanza kuingia kwenye mfumo, goli mbili mfululizo kwenye mechi mbili tofauti, hiyo ni hatua kubwa kwake.

Bila kusahau kuwa nguvu ya Liverpool kwenye kushambulia ilikuwa kwa mabeki wa pembeni, yani Alexander Arnold na Andy Robertson, nguvu hii ilipotea kabisa baada ya Alexander Arnold kushuka kiwango, lakini sasa anaonekana kurudisha kiwango chake.

Kwa mabadiliko hayo, nategemea kuona Liverpool ikiendeleza ushindi kwenye mechi zifuatazo.


1676897132373.png