Liverpool kufuta uteja mbele ya Madrid leo?

Feb 7, 2023
61
36
5
Usiku wa leo itapigwa mchezo wa ligi ya Mabingwa ulaya kati ya Liverpool dhidi ya Real Madrid kwenye dimba la Anfield.

Mchezo unaotazamiwa kuwa mkali na wakuvutia kutokana na ubora wa Liverpool kwa mechi za hivi karibuni na kurejea kwa baadhi ya nyota wao Van Djik, Jota na Firmino.

Kwenye michezo mitano ya mwisho kati ya timu hizi, Madrid ameshinda mechi 4 na sare moja huku mchezo wa mwisho kukutana ilikuwa tarehe 28/5/2022 kwenye fainali ya UEFA na Madrid kushinda goli 1-0.

Je, Liverpool akiwa ndani ya dimba lake la Anfield atafuta uteja mbele ya Madrid ya Benzema, Vin Jr, Modric na Rodrygo?Screenshot_20230221-092931_Twitter.jpg
 
  • Like
Reactions: Zaka