Magoma Na Mwaipopo Waangukia Pua Kesi Dhidi Ya Yanga

Kijiweni

Administrator
Staff member
Nov 7, 2022
281
396
25
Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imetupilia mbali rufaa ya Juma Ally Magoma na mwenzake Geofrey Mwaipopo waliyokuwa wameikata dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Klabu ya Dar es Salaam, Young African Sports, maarufu kama Yanga.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu, Septemba 9, 2024 na Naibu wa Mahakama hiyo, Livini Lyakinana kwa niaba ya Jaji Mfawidhi, Salma Maghimbi aliyeisikiliza rufaa hiyo
Magoma na Mwaipopo walikata rufaa hiyo mahakamani hapo wakipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Dar es Salaam, Kisutu kuiongezea Bodi ya Wadhamini ya Klabu ya Yanga na wenzake muda wa kufungua shauri la maombi ya marejeo.

Yanga iliomba kuongezewa muda huo ili kufungua shauri hilo la marejeo ya hukumu ya mahakama hiyo iliyobatilisha Katiba yake ya sasa kufuatia kesi ya msingi iliyofunguliwa na Magoma na mwenzake, wakihoji uhalali wa katiba hiyo.

Wajibu rufaa katika rufaa hiyo walikuwa ni Bodi ya Wadhamini ya Klabu ya Yanga (mjibu rufaa wa kwanza), Fatma Abeid Karume (mjumbe wa bodi hiyo mpaka sasa), Abeid Abeid na Jabiri Katundu, ambao pia waliwahi kuwa wajumbe wa bodi ya klabu hiyo.

Bodi ya wadhamini wa Yanga imewawekea pingamizi la hoja za kisheria kina Magoma dhidi ya rufaa hiyo, ikibainisha hoja mbili. Kwanza inadai kuwa uamuzi ambao kina Magoma wameukatia rufaa na ya pili wanadai kuwa rufaa hiyo imeshapitwa na tukio.

Pingamizi hilo lilisikilizwa Agosti 30 mwaka huu, ambapo mawakili pande zote Kalaghe Rashid wa Yanga na Jacob Mashenene wa kina Magoma walichuana kwa hoja za kisheria kila mmoja akijitahidi kuishaiwishi mahakama ikubaliane nao na kurejea kesi mbalimbali kusisitiza hoja zao.

Hata hivyo Mahakama katika uamuzi wake imetupilia mbali rufaa hiyo baada ya kukubaliana na pingamizi la Yanga kuwa uamuzi waliokuwa wanaukatia rufaa haukuapaswa kukatiwa rufaa kwa mujibu wa Sheria.