Man United Tunashukuru tumeshinda Na ugenini pia

Brenda

Mgeni
Oct 31, 2022
489
403
5
Dar es salaam
Maguire kacheza Vizuri sana wadau, tumpe sifa anayostahili anapofanya Vizuri, alituokoa Na block moja ingepita sidhani kama De Gea angedaka

De Gea nae alituokoa bao moja la kichwa sijui ilikuwa kona ile amefanya Vizuri, kwa Mara ya kwanza nimeona De Gea footwork iki improve.

Casemiro ndio Backbone ya Team kwa sasa, Spanish Teams zilikuwa zinatusumbua kwa sababu tukipata mpira ilikuwa tunarukaruka unarudi kwao tena, Casemiro anaituliza team, pia south America players wanajua sana kukaa Na mpira Na kutuliza team wanatusaidia

Erik Ten Hag anajua.So far anafanya Vizuri, padogo alipofeli ni quality ya wachezaji

Fred hawezi kukupa zaidi ya afanyacho,hawezi kukupa Ziada, anamuangusha sana Kocha kupata kilicho bora zaidi

Weghorst hata kupiga mashuti mpira haukai mguuni, akipiga lazima aanguke chini Nadhani adui yake mkubwa ni body Mass yake yeye mwenyewe, size kubwa sana ile kwa mpira wa miguu

Malacia Jana kacheza kwa ukamilifu sana, sikupenda acheze Lakini kacheza Vizuri kwa kiwango cha juu labda kwa vile Spanish Teams always walaini Na yeye mlaini

FrXh9GUXgAAaml7.jpg